Kiswahili endelevu

Sadakta! Tumakinike tena kwenye ulingo huu wa lugha yetu tunayoitukuza. Leo tutaangazia makosa ambayo yame’boreshwa’ kwenye maongezi ya kileo mpaka kiswahili kinaborongwa na kuharibiwa kwa upeo mkubwa! Makosa hayo yamebuka kuwa mengi na hatuwezi kuyaangazia yote japo kwa kiasi fulani kwenye kila fursa.

Makosa ya usemi wa kileo:

-Ni makosa kutimia kiambishi 'ju’ ukikusudia kumaanisha 'kwa sababu’. Kwa mfano ni makosa kusema ‘Nimechelewa ju nililala sana’.
Usahihi ni kutumia maneno; Kwa ajili, kwa sababu, kwa kusudi, au kwa minajili. Kosa hili limekidhiri sana kwenye kizazi cha sasa.

-Hatutazami na macho bali tunatazama kwa macho.
-Hatusemi ‘Mtu mgani?’ Twasema ’ Mtu yupi?’ Neno ‘gani’ ni kiambishi tasa na hakiambatanishwi na kivumishi chochote haswa tukielezea juu ya Mtu au watu. Mfano kama huu tena ni twasema ‘Mwanafunzi safi na wala siyo Mwanafunzi msafi’.
-Neno 'mnene’ hutumiwa tu kwa mwanadamu kwa mfano ’ Juma ni mnene kuliko Jese’. Nano ‘mnono’ hutumiwa tu kuashiria wanyama.Kwa hivyo likitumiwa kuashiria mwanadamu ni matusi.

  • Kama nilivyoeleza hapo juu kwenye mfano was Juma na Jese, uyaona nilivyowafananisha. Hatusemi 'Juma ni mnene kumliko Jese bali twasema Juma ni mnene kuliko Jese.
    Tutaliendeleza hili somo kwenye sehemu yake ya pili katika vipindi vijavyo.

CHEMSHA BONGO
-Hawa ndege waitwaje kwa kiswahili?
i) Peacock…
ii) Flamingo…
iii) Guinea fowl…
iv) Honey bird…
v) Heron…
vi) Wood Pecker…
vii) Falcon…
viii) Eagle…
ix) Jiko la makaa huitwa aje kwa Kiswahili?
x) Pulpit ni nini kwa Kiswahili?
Hayo ni maswali mboga kabisa kwa Leo. Jikakamueni.

Msemo wa Leo. Mchimba kisima huingia yeye mwenyewe!

Shukrani za dhati kwenu nyote wanakijiji.
[B]

[/B]

6 Likes

) Peacock…-----------------> Tausi
ii) Flamingo…--------------> Flamingo
iii) Guinea fowl… -----------> Kanga
iv) Honey bird… ------------>
v) Heron…-------------------> Korongo
vi) Wood Pecker…---------->
vii) Falcon…------------------>
viii) Eagle…-------------------> Tai
ix) Jiko la makaa huitwa aje kwa Kiswahili?
x) Pulpit ---------------------> Mimbari

2 Likes

Peacock - tausi
Eagle- mwewe
Guinea fowl-kanga
Izo zingine @mukuna atajibu

1 Like

Asante kwa kuangazia haya makosa. Tutafanya juhudi kurekebisha na kukosoa.

i) Peacock… Tausi
ii) Flamingo…
iii) Guinea fowl… Kanga
iv) Honey bird… chozi
v) Heron… Mbuni ?
vi) Wood Pecker… msumbua miti
vii) Falcon… Mwewe
viii) Eagle…
ix) Jiko la makaa huitwa aje kwa Kiswahili?
x) Pulpit ni nini kwa Kiswahili?

Wengi wetu msamiati wa nyuni tulipata hapa

1 Like

@Meria Mata chukua hii TBT.

Jaribio zuri.

1 Like

Greenhouse inaitwaje kwa oswahili?

1 Like

Nyumba ya kijani

1 Like

cc @kush yule mnono

3 Likes

Asante Sana at mwalimu @xuma lakini Leo sina jibu ila peacock…> tausi

1 Like

Leo imekua ngumu

1 Like

Na juu yeye ndie alijitusi, hapo sawa kush yule mnyama

2 Likes

Kongole!

1 Like

Ni kuongeza jitihada kaka.

Sitaki kukupa jibu lisilo sahihi kaka kwa sasa kwa sababu sijakutana na matumizi ya hilo jina kwa kiswahili lakini nitakujibu baada ya si mda.

Mbona umeboronga lugha kwa kurudia lile kosa nililoangazia hapo awali kaka? Matumizi mabaya ya neno ‘ju’.

:D:D:D:DMazoea ni utumwa kaka

1 Like

MAJIBU YA LEO:
CHEMSHA BONGO

-Hawa ndege waitwaje kwa kiswahili?
i) Peacock…Tausi. Kongole @Nottybwoy , @Mjuaji ,@TerribleWaste na @Chifu
ii) Flamingo…Heroe
iii) Guinea fowl…Kanga. Kongole @TerribleWaste , @Mjuaji na @Chifu
iv) Honey bird…Keremkerem
v) Heron…Koronga
vi) Wood Pecker…Kigogota
vii) Falcon…Kozi
viii) Eagle…Tai. Kongole @TerribleWaste
ix) Jiko la makaa huitwa aje kwa Kiswahili?..Seredani
x) Pulpit ni nini kwa Kiswahili?..Mimbari. Kongole @TerribleWaste
Maswali ya Leo yamekuwa kizungumkuti kwa wengi lakini natumai tumejifunza mapya. Kongole kwa wale wote walioshiriki na waliochungulia dirishani kama kina @4makind , @vuja de ,@sludgist , @introvert ,@jumabekavu na wengineo. @123tokambio kwani Leo uligonga ukuta?

Laleni unono na si unene.

Shukrani za dhati kwenu nyote wanakijiji.

3 Likes

:D:DJinasue kutoka huo utumwa kaka.