Chinda ya matamuchi
Umegonga ndipo!:D:D:D:D:D
CHIEF , SI MWIGIZAJI ? AMA NI KILUHYA HAPO UMEANDIKA
Jaribio Zuri kaka. isipokuwa Install kakupiga chenga lakini maelezo yako ya Paa ni sawa kabisa!
Kwenye mnyambuliko wa vitenzi, neno ‘Igiza’ laweza kunyambuliwa kama [COLOR=rgb(255, 0, 0)]mwigaji au mwigizaji au mwigishaji. Shukran.
ahsande kumbe najua kiswahili
samaki hupalwa ama hupaluliwa magamba hivyo, maana zilizobakia za neno PAA ndizo zenyewe…
MAJIBU YA LEO
CHEMSHA BONGO
[B]i)Blackmarket…Soko haramu au Magendo. Kongole @IsMundu @bababibitoto na @gashwin
ii)Accountability…Uwajibikaji. Kongole @gashwin ,@bababibitoto na @IsMundu.
iii)Install…Tawaza/weka/tawalisha/ingiliza (hili lilikuwa kizungumkuti)
iv) Surf(the internet)…Rambaza (hili nililiuliza baada ya ule mjadala tuliokuwa na @123tokambio na @Kamu asubuhi ya leo)
v)Workshop…Karakana/warsha/Hafla. Maana ya kwanza ni ‘gereji’ na ya pili na tatu ni ya mkutano. Kongole @gashwin , @bababibitoto na @IsMundu .
vi)Sycophannt…Mpanda au kibaraka. Shukran @bababibitoto
vii)Maana tatu au zaidi ya neno ‘Paa’.
-Mnyama ambaye wakati mwingine huitwa Swara.( @gashwin hapo ndipo shida ilikuwa)
-Sehemu ya juu ya kuezekwa ya nyumba.
-Kuruka na kuelea angani. Kongole kwa akina @bababibitoto ,@gashwin na @IsMundu lakini kuna dosari moja;wakati wa kuelezea maana ya neno fulani ni vizuri kuelezea ukiepuka kulitumia neno lilelile kwenye maelezo yako.
Kina @ziegler , @uwesmake ,@Meria Mata , @mpotorico , @Kamu , @Liberty na @123tokambio shukran kwa kushiriki.
Nawaacha na Msemo: Safari ya mbali, huanza na hatua moja ; na pia vilevile, Bandu bandu huisha gogo.[/B]
[B]
Shukran.[/B]
[/QUOTE]
Kibaraka nilifikiria lakini nikaona kidogo ni kama ina mushkhil. Doh!!
PANYA MIJINGA @Mtanzania Magufuli KUJA UFUNZWE KISWAHILI
@xuma kabla uodoke. eleza “Bandu bandu huisha gogo.”
Nipo kaka na ninashukuru kuwafunza hawa shoga zangu Kama @uwesmake wajifunze matwana la Kiswahili sanifu
Yamaanisha ukiwa na ari jambo lolote hata liwe kubwa au zito aje utalimaliza au utapata suluhu yake. Msemo huu hutumiwa kujipa moyo. Unawiiana na ule wa ’ kidogo kidogo hujaza kibaba’. Gogo ni kipande cha mti uliokatwa na bandu ni ile hali ya kuupasua kwa vipande vidogo vidogo vya kuni ukitumia shoka. Kwa hivyo kila ukipasua(bandu) gogo hilo lapunguka na baada ya muda linaisha!