Kiswahili Endelevu

Kwa wapenzi wa lugha hii tukufu, ni vyema tuwe tukinoa makali ili kuuondoa ubutu unaoweza kuisambaratisha lugha makinifu. Tutatumia uchanjaa huno kuelimishana na vile vile kuburudika. Walio na maswali watajibiwa na yeyote awaye yule na ufahamu wake. Kina @mukuna na magwiji wengine karibu.

Msamiati wa leo

-Toothpick kwa kiswahili ni kichokonoa.(Hii ni kwa sababu hutumiwa kuchokolea mabaki ya chakula kwenye meno).

Chemsha Bongo

Tafsiri ya haya maneno kwa kiswahili;
-Implements…
-Bacterium…
-virus…
-Accord…
-Avocado…

2 Likes

Avocado … Ofokado. Hiyo do mimi najua

5 Likes

Implements - Zana

Bacterium - Vimelea

Virus - Virusi

Accord - Mkataba

Avocado - Parachichi

9 Likes

Nisaidiwe hapa tafadhali.
Tap - …
Pipe -…
Canal -…
.
Asanteni in advance

2 Likes

Tap-bomba
Pipe- mfereji
Canal-
[FONT=Georgia][SIZE=2]Kiswakingi kifkuzwe[/SIZE][/FONT]

tap-fereji
pipe-bomba
canal- mtaro

5 Likes

Who has a marking scheme?

1 Like

@xuma

1 Like

@xuma ebu acha kisokonkwinyo kidogo uje hapa usaidie

1 Like

@Mtanzania Magufuli hebu changia

Huyo ni ghushi, kavaa kilemba cha ukoka.

1 Like

Ukoka ni nini?
Sounds like mugoka in singular form

3 Likes

kuvaa kilemba cha ukoka ni kuwahadaa waja kwa kujitunuku hadhi usiyo nayo.

4 Likes

Heheh…I bet ukoko ni ile naita mùkùrì in Greek

1 Like

Kiswahili kimenipiga chenga, sijashika kitu

Unaousema wewe ni ukoko (crust). Ukoka ni aina ya nyasi (reeds). kilemba cha ukoka literally means a turban made of reeds. Figuratively it means something inferior that is not what it purports to be.

6 Likes

Shuran, sasa nimepata.
Pewa faxe mbili ntalipa

1 Like

Nimewasili kakangu.

1 Like

Avocado so kodofia?

1 Like

Tap…Mfereji
Pipe…bomba au fereji(kutokana na ukubwa kuliko mfereji)
Canal…Mkondo au mtaro mkubwa. Pia vilevile hutwa mfereji mkubwa. Kwa mfano; Mfereji wa Panama, Mfereji wa Suez.
NB. Kumbuka yote tatu ni mifereji(njia ya kupitia maji) lakini inatofautishwa tu na udogo au ukubwa wake).

2 Likes