Kiswahili Endelevu

Misamiati ya leo

-Mouse (ile ya tarakilishi au kipakatalishi) huitwa puku au kipanya.

-Website ni tovuti.
-Internet ni Mtandao.
-Browse ni vinjari na kadhalika na kadhalika.

Chemsha Bongo

-[B]Tafsiri maneno yafuatayo kwa kiswahili;

i) Hiccup…
ii) Apple…
iii) Appliance…
iv) Gadget…
v) Forum…
vi)Handcart…

N/B.Twashukuru maulana, muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo kwa kutuwezesha kuiona Jumapili nyingine. Waja wa dini ya kikristo ni siku nyingine ya kumuabudu Jalali.[/B]

Asante Mwanakijiji Mkuu Bw @xuma
Kutoka leo sitochanganya matumizi ya maneno ‘tovuti’ na ‘mtandao’.
Kwa sababu mimi ni Mkenya halisi siwezi tafsiri hayo maneno bila usaidizi wake Google.

hiccup… Kwikwi

leo naangalilia mbali

Appliance - kifaa
Hizo zingine @emali ameJibu

gadget-kifaa
handcart-mkokoteni
forum-jukwaa

handcart- wogeni

gadget-burungo

vi)Handcart…Rukwama

Hapo sawa kaka.

Umegonga ndipo kaka.

:D:D:D:D:D

Gadget ni sawa lakini kuna jina lingine halisia. Handcart: umenoa: Forum umeng’amua.Kongole!

leta majibu

Hapo sawa. Lakini kuna jina lake lingine halisia. Kongole.

Unajitosa ulingoni kwani kupotea njia ndiko kujua njia kaka mkubwa.

Ndiyo haya basi.

iv) Gadget…Kidude

MAJIBU YA LEO

Chemsha Bongo

-[B]Tafsiri maneno yafuatayo kwa kiswahili;

i) Hiccup…Chechevu/Kekeru/Kikwifukwifu/Kitefutefu/Kwikwi. Hongera @4makind ind kwa kupata jibu sahihi.
ii) Apple…Tofaa au Matofaa kwa wingi. @emali , kongole kwa kupata hili.
iii) Appliance…Ala au kwa wingi Nyala
iv) Gadget…Kidude au Kifaa. Kongole @Meria Mata, na @weston kwa kung’amua hili.
v) Forum…Ukumbi au jukwaa lakini jina jukwaa mara nyingi humaanisha ‘stage’. @Weston na @emali kongole.
vi)Handcart…Rukwama. Kongole @123tokambio kwa jibu sahihi.

@kender9 [/B]Shukran kwa kushiriki japo hugugonga ndipo.

Nawaacha na msemo ‘Mfa maji haachi kutapatapa’.