Kwa wapenzi wa lugha hii tukufu, ni vyema tuwe tukinoa makali ili kuuondoa ubutu unaoweza kuisambaratisha lugha makinifu. Tutatumia uchanjaa huno kuelimishana na vile vile kuburudika. Walio na maswali watajibiwa na yeyote awaye yule na ufahamu wake. Kina @mukuna na magwiji wengine karibu.
Msamiati wa leo
-Toothpick kwa kiswahili ni kichokonoa.(Hii ni kwa sababu hutumiwa kuchokolea mabaki ya chakula kwenye meno).
Chemsha Bongo
Tafsiri ya haya maneno kwa kiswahili;
-Implements…
-Bacterium…
-virus…
-Accord…
-Avocado…
Unaousema wewe ni ukoko (crust). Ukoka ni aina ya nyasi (reeds). kilemba cha ukoka literally means a turban made of reeds. Figuratively it means something inferior that is not what it purports to be.
Tap…Mfereji
Pipe…bomba au fereji(kutokana na ukubwa kuliko mfereji)
Canal…Mkondo au mtaro mkubwa. Pia vilevile hutwa mfereji mkubwa. Kwa mfano; Mfereji wa Panama, Mfereji wa Suez.
NB. Kumbuka yote tatu ni mifereji(njia ya kupitia maji) lakini inatofautishwa tu na udogo au ukubwa wake).