KINACHOIPOTEZA TZ HIKI HAPA

TUNAIGIZA MAISHA YA KIJAMAA KWENYE TANZANIA YA KIBEPARI.
Habari great thinkers,
Kwanza poleni wana JF wote ambao tyumefanyika kuwa wakimbizi wa kimtandao, Mimi ni mkimbizi mwenzenu ninayeishi uhamishoni nchini kenya kimtandao. nikienda moja kwa moja kwenye mada yenye kichwa tajwa hapo juu, nadhani aina ya social-political formation ambayo tunaifata Tanzania nayo ni kikwazo katika kutufikisha mahala ambapo ni bora zaidi ukilinganisha na tulipotoka.
Aina ya social-political formation ambayo tunaifata Tanzania nashindwa kuielewa hadi leo maana yake kwenye katiba tunaambiwa kwamba Tanzania ni nchi ya kijamaa lakini kiuhalisia sisi tunafuata ubepari. Sheria nyingi za Tanzania zingefaa zaidi kama tungekuwa ni wajamaa pure lakini zinaonekana kuwa hazifai na kandamizi kwa sababu zinaongoza nchi ya kibepari, nitatoa mifano michache

  1. Hivi karibuni serikali iliweka figisu figisu kwa Klabu ya soka ya SIMBA ili[potaka kumpatia mwekezaji asilimia 51 za hisa za klabu ili awe na final say kwa mambo yanayohusu klabu, hili liligonga mwamba baada ya Waziri mwenye dhamana ya michezo kuwazuia kwa kuwa sheria hairuhusu mtu mmoja kupewa zaidi ya 49%, hii inaonyesha wazi kwamba jinsi serikali na sheria zake zinavyo discourage private ownership na maendeleo kwa ujumla katika soka kwa sababu tunaigiza maisha ya kijamma kwenye Tanzania ya kibepari.
  2. Sakata la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, Tanzania ukisomea shule binafsi ni kosa la jinai na hupaswi kupatiwa mkopo (mimi mwenyewe ni victim wa hii inshu maana nimeomba mkopo mara 3 mfululizo na nimenyimwa kwa sababu form 5 na 6 nimesoma private na mara zote sababu za kuninyima ni kwamba nimesomea A-level shule binafsi)
    Hizi ni baadhi tu ya mifano halisi ambayo nimepata muda wa ku share nanyi ndugu zangu kutokana na muda nitaishia hapa na nitaendelea ku update kila nipatapo muda, nanyi ndugu zangu mnaweza kujazia jazia hapo.
    WASALAAM, Mwanachama mnazi wa JF

Rudi darasani katafute historia ya SIMBA ndo urudi kurekebisha uzi wako kuhusu suala la ‘Kwanini asilimia 49, na si zaidi?’

Kwa nini usiweke hapa unachokijua ili naye apate kuelewa? Mtoa uzi kaandika anachokijua hivyo kama wewe unakijua kitu tofauti tuwekee hapa tusome. Tatizo lako wewe unataka kila kitetea buku7 yako

Kinachoisumbua tanzania ni fikra za kijamaa za wana ccm, ujamaa unaenda pamoja na udikteta, ujinga, uvivu, uwoga na umasikini. Katiba mpya iliyo bora ndio mwarobaini lakini kwakua ccm wanajua hawawezi ku survive kwenye dunia yenye ushindani wa kweli ndio maana wanakumbatia mifumo ya kizamani isiyo na matunda.

samahani ndugu yangu inawezekana ikawa ni kweli un uelewa mkubwa kunizidi labda lakini jikite kwenye kuelewa mantiki ya hoja na sio sentensi moja moja…
nilipotolea mfano wa SIMBA, hio ni moja ya mambo mengi ambayo yanadhihirisha kuwa TZ tunaishi maisha ya kijamaa ndani ya ubepari kwa sababu nachokifahamu mimi ni kwamba, kilichozuia mwekezaji wa simba asipewe 51% ni sheria ndo inakataza na sio vinginevyo.

kabisa ndugu yangu

SHERIA HII IMEFANYIWA MAREKEBISHO OKTOBA 2017 ILI KUZUIA MTU ASIMILIKI HISA 51%

Baada ya mfanya biashara Mohammed Dewji MO kushinda zabuni ya uwekezaji ndani ya klabu ya Simba ambapo kutakuwa na mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kutoka uanachama hadi hisa, mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa kuhusu asilimia za hisa atakazopewa tajiri huyo na zile ambazo zitabaki kwa wanachama.

Msajili wa vyama vya michezo Ibrahim Mkwawa ametoa ufafanuzi juu ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kwa vilabu vilivyoanzishwa na wanachama kwenda kwenye mfumo wa hisa kama ilivyofanya klabu ya Simba.

[COLOR=rgb(243, 121, 52)]Msajili huyo ameeleza kwamba, kanuni mpya za serikali zilizotoka mwezi October 2017 zinaeleza kwamba mfumo wa hisa ni asilimia 51 kwa 49.

“Kanuni hizi baada ya kutangazwa zimeshakuwa sheria na kwa mujibu wa kanuni hizi, kanuni ya 28 (a) (i) inasema kwamba, vilabu ambavyo vimeanzishwa na wanachamavikitaka kuuza hisa zake vinapaswa kutenga asilimia 51 kwa ajili ya wanachama wake na asilimia 49 kwa ajili ya mwekezaji. Kanuni ndio ziko hivyo, na kanuni kanuni hizo kabla ya mkutano mkuu zilipelekwa klabu ya Simba na wao wanazifahamu.”

“Kwa hiyo ni kitu ambacho kipo kwenye kanuni mabadiliko yake sasa hilo ni suala jingine lakini kwa sasa tunakwenda na 51 kwa 49.”

“Wao kama hawakuliweka wazi siku ya mkutano, mimi siwezi kulisemea walipaswa wawaambie wanachama wao lakini kimsingi walikuwa wanalifahamu.”

“Si dhani kama kutakuwa na mgongano kwa sababu ule ulikuwa utaratibu tu wa kumtangaza mshindi sio kwamba ndio amepewa hisa asilimia 50, kinachofuata sasa ni taratibu za kisheria ambazo moja kwa moja zitaangukia kwenye kanuni ambazo zimeshatungwa kwa hiyo hakuna mgongano wowote.”

“Wanachama na mashabiki wa mpira waelewe kwamba, serikali sasa imeshatunga kanuni ambazo itaziongoza klabu zote sio Simba tu, klabu zote za mpira wa miguu ambazo zinamilikiwa na wanachama kanuni sasa ziko tayari kama zinataka kwenda katika mfumo huu wa uendeshaji kwa njia za hisa, wazisome kanuni ambazo zimetungwa na serikali ambazo zinawataka wanachama wamiliki asilimia 51 na wawekezaji asilimia 49.”

Mitaani kumekuwa na mijadala mingi kuhusu asilimia za hisa kati ya MO na wanachama, wapo wanasema MO atamiliki 51% halafu wanachama watabaki na 49%, wapo wanaodai kila upande utakuwa na umiliki sawa yaani 50% kwa 50% lakini tayari serikali imeshaweka mambo sawa.

Nakazia

Baada ya mfanya biashara Mohammed Dewji MO kushinda zabuni ya uwekezaji ndani ya klabu ya Simba ambapo kutakuwa na mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kutoka uanachama hadi hisa, mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa kuhusu asilimia za hisa atakazopewa tajiri huyo na zile ambazo zitabaki kwa wanachama.

Msajili wa vyama vya michezo Ibrahim Mkwawa ametoa ufafanuzi juu ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kwa vilabu vilivyoanzishwa na wanachama kwenda kwenye mfumo wa hisa kama ilivyofanya klabu ya Simba.

[COLOR=rgb(184, 49, 47)]Msajili huyo ameeleza kwamba, kanuni mpya za serikali zilizotoka mwezi October 2017 zinaeleza kwamba mfumo wa hisa ni asilimia 51 kwa 49.

“Kanuni hizi baada ya kutangazwa zimeshakuwa sheria na kwa mujibu wa kanuni hizi, kanuni ya 28 (a) (i) inasema kwamba, vilabu ambavyo vimeanzishwa na wanachamavikitaka kuuza hisa zake vinapaswa kutenga asilimia 51 kwa ajili ya wanachama wake na asilimia 49 kwa ajili ya mwekezaji. Kanuni ndio ziko hivyo, na kanuni kanuni hizo kabla ya mkutano mkuu zilipelekwa klabu ya Simba na wao wanazifahamu.”

“Kwa hiyo ni kitu ambacho kipo kwenye kanuni mabadiliko yake sasa hilo ni suala jingine lakini kwa sasa tunakwenda na 51 kwa 49.”

“Wao kama hawakuliweka wazi siku ya mkutano, mimi siwezi kulisemea walipaswa wawaambie wanachama wao lakini kimsingi walikuwa wanalifahamu.”

“Si dhani kama kutakuwa na mgongano kwa sababu ule ulikuwa utaratibu tu wa kumtangaza mshindi sio kwamba ndio amepewa hisa asilimia 50, kinachofuata sasa ni taratibu za kisheria ambazo moja kwa moja zitaangukia kwenye kanuni ambazo zimeshatungwa kwa hiyo hakuna mgongano wowote.”

“Wanachama na mashabiki wa mpira waelewe kwamba, serikali sasa imeshatunga kanuni ambazo itaziongoza klabu zote sio Simba tu, klabu zote za mpira wa miguu ambazo zinamilikiwa na wanachama kanuni sasa ziko tayari kama zinataka kwenda katika mfumo huu wa uendeshaji kwa njia za hisa, wazisome kanuni ambazo zimetungwa na serikali ambazo zinawataka wanachama wamiliki asilimia 51 na wawekezaji asilimia 49.”

Mitaani kumekuwa na mijadala mingi kuhusu asilimia za hisa kati ya MO na wanachama, wapo wanasema MO atamiliki 51% halafu wanachama watabaki na 49%, wapo wanaodai kila upande utakuwa na umiliki sawa yaani 50% kwa 50% lakini tayari serikali imeshaweka mambo sawa.

http://shaffihdauda.co.tz/2017/12/06/ufafanuzi-asilimia-atakazopewa-mo-baada-ya-kushinda-zabuni-simba/

CCM wanataka kutawala kwa muda mrefu na ukitaka kufanikisha hilo SIMPLE minya uhuru wa kupashana habari ili watu wabakie mbumbumbu; hata hutu tu jukwaa twetu twa kijanii nato wametufunga maskini…

Lakini kushindana na Technology ni kazi kubwa mno ni sawa na kumchunga mkeo wakati kitendea kazi chake anayembea nacho muda wote aendako…

na njia nyingine ni kuhakikisha kwamba wanapta elimu mbovu kbs ili wajinga wawe wengi

tunaigiza sana

Point. Katika vitu vilivyodumaza uchumi wa Tanzania ni sera za kipumbavu zinazoitwa ujamaa. Ujamaa umeambatana na uvivu lakini zaidi wivu tena wa kupindukia. Pili usiri wa ajabu, ndo maana mashirika ya umma hayana sifa za kuuza hisa zake kwenye soko la hisa kwa sababu mahesabu yake yamegubikwa na usiri wa kutisha. Hizo siri mara nyingi huficha wizi wa kitaasisi. mfano unakuta CCM imeiba TTCL, au PPF, au Posta. Ili kuendelea kulinda uchafu huo, lazima kila kitu kiwe siri.

Tumefika hapa kutokana na ushenzi kama huu.