KenyaTalk itasababisha JF tz kurudishwa kwa shingo upande

Huku watu wanapiga nondo kisawasawa.
Uhuru huku ni mkubwa, hakuna Monopoly au Censorship.
JF tz hata ikirudi lazima itaweka FILTER ya post zenu.
Ushauri.
Kenya Talk waondoe jina la JF humu kumuenzi Max Melo. Waandike Bongo Forum au Tanzania Forums.

Hapo kuna mawili!!kama jf itarudi hewani kwa kukubali mashariti ya tcra,hasa lile la wachangiaji wake watumie majina halisi ili wajulikane,tayari umaarufu wake utakuwa haupo tena!!na kama hawa ndugu zetu wa kenyatalk wataamua kufungua jukwaa jipya kwa watanzania tu basi jf itakufa natural death!!watu wengi watabaki huku huku,na hata ikirudi rasmi bado watu watakuwa wanaingia kimachale machale labda kuna mtego umewekwa!!hivyo nashauri uongozi wa jf wawe makini ktk kutatua dhahama hiyo!!

Haswaaaaa

Naamini JF zote mbili zinaweza kubaki na zote zikafanya vizuri

Mimi nashauri hii jf ya KT ibaki kama backup ya huku hm maana Tz kuzingua ni lazima. Mnakumbuka wakati wa uchaguzi jamaa walizingua? Huku KT itakuwa ni sehemu reliable za kupeana taarifa muda wote. Hofu na shinikizo kwa baadhi ya post ni kubwa jf Tz. Hivyo huku zitajadiliwa bila hofu. Inapaswa jf Tz ikirudi tuwaambie members wote kuwa wakiona jf Tz inazingua wanahamia huku mara moja, na ikibidi kwa id zao original.

Haswaaa kiongozi. Nakubaliana nawe.

Tupende tusipende,Kenya talk ni mkombozi wetu katika nyakati za masahibu. Uhuru pia ni 100%

Kenya talk ibakie hivi hivi, kule Tutaremb huku tutaweka nondo za ukweli

Mbona mimi sijaona nondo ya uhakika iliyowekwa huku?

“WAKUU” bado wanapima kina cha maji!

Watch the space, mbona una haraka?

ushawahi kurudi kwako huku ukinyata? hilo ndilo linalotusibu kwa sasa

Wazo zuri TF itafaa

wakuu hivi KT haipo App Store?