kenyan thuggery

Hii Nairobi yetu manze kila msee ni mwizi kila mtu anataka kukuibia na sijui hii culture ya wizi ilitoka wapi meen.

A few years ago kuna vidaa ilikuwa inatrend online. I think ilikuwa sides za Molo ama Naivasha mahali wanauza viazi kando ya barabara. Kuna msee alikuwa anadai kubuy viazi alishuka gari alafu kuenda kushika ile viazi iko kwa ndoo ikaanguka yote na ndani. Hao wasee wa kuuza kuna vile waliondokea iyo place vibaya sana. Walidhani uyo msee ni karau amekam kuwashika. Hao wasee walikuwa wanabalance viazi kwa ndoo inakaa ni kama ndoo imejaa kumbe huko chini hakuna kitu. Unabuy viazi unapata hakuna any manze. Staying on potatoes, ukienda kubuy viazi nimenotice tabia flani, hao watu wa kuuza viazi wanaeka viazi kubwa juu alafu uko ndani wanakuekea viazi ndogo bana. Unabuy viazi ukifika home bana unapata ni tule tudogo hata huezi toa ngozi juu ukitoa ngozi kanaisha bana.

Ukienda kubuy mahindi, wanakuuzia mahindi na gorogoro lakini gorogoro yenyewe manze imekatwa half. Wizi wa hali ya juu. Gorogoro ni 2kg lakini ukipima afta umeekewa haifika hata 2kg manze.

Ukienda kubuy mbao pale kwa timberyard jamaa wa kukuuzia ameinterfere na measuring tape intentionally. Instead ya measuring tape kuanzia 0 ya uyo msee inaanzia 1. Unanunua mbao ukienda kufit kwa nyumba haiingiani bana. Ukisuggest kutumia measuring tape yako huyo msee anakwara ati yake pia iko sawa. Mkora kabisa.

Kuna pia zile lorry za kubeba mchanga na kokoto uko Ruai na Kamulu, hao majamaa huko chini wameeka mabati flani bana unapata wanabeba mchanga less. Instead ya 10 tonnes jamaa anakuletea 7 tonnes na bado ng’ombe ya mtu inakulipisha 30k malaya za watu hawa.

Ukienda kubuy nyanya, ule mathe wa kukuuzia nyanya kumbe ameongeza kasuku ndogo ndani ya ile kubwa ukibuy nyanya ya soo unapata haifiki. Nyanya za soo in reality unapata ni nyanya za chwani.

Huko Naivasha ukienda Naks, watu wanakuuzia yoghurt mbaya bana. Unanunua yoghurt although we si dereva inabaki tu safari mzima umeendesha mbaya. Kuna siku nilikuwa naenda Western, nishainunua iyo yoghurt iyo njia, we jua iyo safari ilikuwa ndefu walai weeh sitaki kukumbuka.

Unaenda baze ya keg, ukibuy keg uyo mathee anakuekea keg imejaa povu kuruka na mjinga anataka umpee 70 bob bana. Yaani unalipia keg na pia unalipia povu. Iyo cup yote kubwa unapata unakunywa cup nusu tu alafu uyo mathee anakushow hana straw ukunywe na iyo cup ivo ghasia yeye. Na sijai jua kwa nini baze za keg zinakuanga na mamathe wamebeat kuruka. Wako overweight na wanakaa wanyanye.

Alafu ukienda butchery kubuy nyama. Jamaa anacheza na iyo weighing scale yake. Kuanza izi digital wezi kabisa. Nyuma ni 1kg lakini ukipika inakaa nyama quarter bana. Meffi hao watu.

Hii kenya yetu kila mtu ni thug banae. Hata karau anakuanga a thug in uniform. Hope Sugoiman atatusaidia.

True dat

:D:D:Denda butchery nunua kilo moja, alafu enda pima kwa nyumba…

Ukienda pale kanisana mchungaji anataka utoboke pesa mzuri ndivyo akumwagie mafuta na kukuombea.

On point…lakini watu wa garage aka mechanic ni kama ume wa sahau. Very god fearing people.

Enda pale brothel kahaba anakuambia uongezee pesa kwa sababu umekaa sana bila kumwaga.

Sijaona ukibonga pia juu ya broker anakula side zote mbili

Sugoiman ni thug my friend. Aliua Jacob Juma ndio akuwe na monopoly ya ku supply NCPB na mahindi zake kutoka Congo

…basi hujaona ya firauni kaka.
Kuna time on my way home, hizo sides za
Githurai kuna hawa wasee wa kuuza miwa Kwa jwala. Nilishika mbili Moja yangu na wife na hio ingine maboyz wajibambe tukiendanga home.

Bite ya kwanza ilikuwa fiti ya pili ndio ilinimalisa, ghaseer alikuwa amechenganya miwa na tu viazi amechonga…:D:D

Wueh na wizi ya corporates ndio hiyo, unasupply goods ama services kumbe lazima utoboke kila mahali, soldier, accounts office, board uwajenge pia leading to rising cost of the goods supplied. Shinda wanataka wewe usupply na Ile bei ya chini kabisa lakini bado uwajenge unawaambia wajidinye

Kisha kuna rustler; anaongojea umechunga ngombe na mbuzi zako all your life; alafu ghasiaa inakuja chukua ivyo tu tena ki mambavu … na akuna kitu unaweza fanya. Hii Kenya aki …

Alafu sasa kuna wale fundi wa laptop tao hehe…unapeleka stuff yako iundwe, anang’oa spare parts kutoka laptop yako unarudishiwa mkebe na hakuna penye utampeleka.

really?,ukisema thats black mail anasema utoe kadudu yako?

Why do you think Kenyans elect thugs as leaders.
Leaders are a reflection of the society. Most Kenyans only complain of corruption because they not the one benefitting

:D:D:D:D

Hii Nairoberry inakaa bado changa kwa wengi sisi.

Alafu kuna pia madaktari hosi. Ulikuwa na homa umeenda kutibiwa jamaa anakuandikia ufanye tests 1 million bana na ni homa tu. Anaeza kuandikia hata ufanyiwe Xray ya mgongo na saa hio ni homa uko nayo. Kwanza kama ukona NHIF na ikuwe we ni civil servant, watanyonya wewe sawasawa.

Unaendanga hosi private wanakuuliza unalipa na nhif? Ukisema ndio wanakusho ulale wakuchunguze shida ni gani :smiley:

MP Shah na Aga Khan wanapenda hii tabia sana

Kenya is rotten to the core. Hapa njiru kuna vichinjio buchariii kilo ni Mia tatu. At first ilikuwa legit. Baadae ukora ikaingia. Watu wakatoroka wote. Nyama siku hizi naendea Kwa woria hao hawana haraam.
I made a personal pledge I would rather loose on my knees than win through crooked ways.

Banae ukisha testiwa wanakuandikia madawa kama Aina tano zingine ukiangalia online unapata ni za kuongeza calcium kwa mwili hata mwenye anakuuzia kwa chemist anaanza kusmile kiholela. Unajua hapa umetiwa stick.