Karaoke Sunday.

Lady ISSA

Ooh mwanangu dunia ina mambo,
sikia maneno,
nakwambiaka,
mupe roho yako Mola wako,
heshima kwa wazazi eee mwanangu.

Dunia hii mama lukumba lukumba,
dunia hii ina mambo mwendo wa ngamia,
dunia hii mama lukumba lukumba,
dunia hii ina mambo mwendo wa ngamia.

Chunga mwenjiyo atakudanganya,
kwa yote ile atapenda yeye,
kipenda roho kila mutu na yake,
yake ni yake na yako ni yako.

Dunia hii mama lukumba lukumba,
dunia hii ina mambo mwendo wa ngamia,
dunia hii mama lukumba lukumba,
dunia hii ina mambo mwendo wa ngamia.

Mwendo wa kobe maele maele,
mwendo wa chui kuwinda winda,
mwendo wa nyoka lukumba lukumba,
mwendo wa ngarama ah njia ya faradhi.

Dunia hii mama lukumba lukumba,
dunia hii ina mambo mwendo wa ngamia,
dunia hii mama lukumba lukumba,
dunia hii ina mambo mwendo wa ngamia.

Tabu na raha inakungojea,
inategemea akili yako,
tafutaaaa eh utapata eh,
kumbuka maneno nakwambiaka.

Dunia hii mama lukumba lukumba,
dunia hii ina mambo mwendo wa ngamia,
dunia hii mama lukumba lukumba,
dunia hii ina mambo mwendo wa ngamia.