Kampuni ya China yaunda tovuti ya urambazaji ya Kiswahili

Jan, 2016 kampuni ya China ya 16Lao imeunda na kuchapisha rasmi tovuti yake ya urambazaji kwa lugha ya Kiswahili. Katika tovuti yao, wamejenga vituo 4 vinavyotumia lugha ya Kiswahili ambazo nivituo vya Kiswahili,Tanzania, Kenya na Uganda.

https://2.bp.blogspot.com/-lG7rHCddCEk/VrP0klUfedI/AAAAAAAAAEs/ZnliACp3axw/s640/Img412042701.jpg

https://3.bp.blogspot.com/-yHTLM__ZceU/VrP0XOUd1cI/AAAAAAAAAEk/LVqR2Yb3IFo/s400/QQ%25E6%2588%25AA%25E5%259B%25BE20160204161518.jpg

Tovuti ya urambazaji inamaanisha tovuti inayokusanya tovuti nyingi mbalimbali kwenye mahali moja na kisha kuainisha kila tovuti kwa aina yake, pia inakusanya habari na taarifa moto zaidi mtandaoni.

Watumiaji wengi wa mtandao nchini China wamezoea kutumia tovuti ya urambazaji kwa ajili ya kutafuta na kuvinjari vituo mbalimbali vya tovuti na kupata kuangalia habari na taarifa zilizokusanyika, na hii ndiyo sababu kampuni hii ya 16Lao imepanga mipango ya kusambaza huduma ya tovuti ya urambazaji kwa Afrika Mashariki.

https://2.bp.blogspot.com/-N9NWG-aJ34E/VrP0hxIQMyI/AAAAAAAAAEo/6pt6wSMNEqE/s640/1114814046_14277624362021n.jpg

Kwenye Kichina, neno “Lao” linamaanisha “kurambaza” au “kukusanya” kwa Kiswahili. Kwa maana kampuni hii ya 16Lao itatoa huduma ya kurambaza data za mitandao ili kurahisishia watumiaji wa mtandao na kutoa jukwaa kwa wenye tovuti ili wapate mahali pa kufanya matangazo.

https://2.bp.blogspot.com/-UKsLbAoa8oU/VrP012g7etI/AAAAAAAAAEw/oSUecBQR9i0/s640/QQ%25E6%2588%25AA%25E5%259B%25BE20160204154311.jpg

Katika tovuti hii ya urambazaji ya Kiswahili kuna sehemu zaidi ya 13 ambazo zinawezesha watu wanaotumia lugha ya Kiswahili wapate tovuti zote zinazochapishwa kwa Kiswahili na habari muhimu ya kila sikuu kwenye sehemu ya habari moto. Pia kwenye sehemu za mkusanyiko wa tovuti watumiaji wanaweza ku pata tovuti zote moto za aina mbalimbali.

https://2.bp.blogspot.com/-BRPOZjeX4C4/VrP1ByaOWfI/AAAAAAAAAE0/oyjpjYH6bYo/s640/QQ%25E6%2588%25AA%25E5%259B%25BE20160204161807.jpg

https://4.bp.blogspot.com/-SNUc9i9t9ig/VrP1BrIzOFI/AAAAAAAAAE4/OPPuuHBGlOQ/s640/QQ%25E6%2588%25AA%25E5%259B%25BE20160204163550.jpg

Zaidi ya mkusanyiko wa tovuti za aina mbalimbali, sehemu zake zingine zimekusanya bidhaa, filamu, michezo na udaku na kadhalika zinazo moto kwenye mtandao.

Kwa ajili ya watumiaji wa Afrika Mashariki kujua na kuanza kutumia tovuti hizi za urambazaji, sasa 16Lao wanafanya bidii. Katika mipango yao ya mwaka huu 2016 watachapisha kivinjari chao mbacho kina toleo za lugha 18, na pia wataendelea kutoa programu za habari na Video, na jukwaa la B2B na B2C.

good post…

Kikingi kizuri…ama ‘Post’ inaitwaje kwa kiswahili:D:D:D:D

5 Likes

mlingoti, tuulize @xuma

Post ni Kuweka

1 Like

kwa hivyo good post itatafsiriwa kama muweko mzuri?

1 Like

Hapo sasa but pia ni neno lenye maana zaidi ya moja unaezatumia ambatisha. i.e ameambatisha vizuri

1 Like

kuiliso tu, urambazaji ni nini? kitabu cha kiswahili mufti nilitupa

1 Like

kuiliso tu, urambazaji ni nini? kitabu cha kiswahili mufti nilitupa

Urambazaji Kiingereza ni Navigation

2 Likes

. Aidha kwa sababu ni kwa mtandao, twaweza fanya utowozi wa moja kaa moja ikawa ’ kipeperushi’ kwa sababu ’ tunaweka’ kwenye mtandao habari peperushi kwa madhumuni ya kuenezwa mtandaoni.

2 Likes

Hongera kwa Wachina.

2 Likes

waar dint know kiswahili was that hard…pliz translate ua listing to english.

ma nigga ,you lost me at tovuti

Oh, I can’t wait to be taught swa by some Chinku. I’d rather my shrubbing teacher from muranga…

hapo ndio china imetufikisha, hata kiswahili?

Tovuti - Website

Nadhan Kati ya hiyo Misamiati ndio imekukanganya kidogo.

Kuainisha – Classifying

Kuvinjari – Browsing

Tovuti - website

2 Likes