Kama hamjui kiswahili Potezeeni!

Ndugu zetu wakenya msikereke kwa kuona ghafla kwenye nchi yenu (Kenyatalk) kiswahili kimetamalaki. Waswahili tuliokuja huku hatukuja kwa mapenzi yetu bali tupo ukimbizini na kiswahili mnachokiona hakizungumzwi kwenye miji yenu (Kenya Forums) bali kinazungumza ndani ya makambi yetu ya wakimbizi.

Bahati tuliyonayo wenzenu ni kwamba Kiingereza cha kubabia tunacho na kiswahili tunacheza nacho kama mwanasesere mikononi mwetu, nyie wenzetu Kiswahili kwenu ni Pasua Kichwa. Vumilieni tu kwani wakimbizi huja na mila na tamaduni za kwao!

Thread kama hizi zimeshakua nyingi sasa

Sijaiona nyingine. Basi Mods waziunganishe. Hatutaki masimango sisi.

Thus why wametuwekea viti huku kwenye chumba kingine, hivyo wakija kwenye chumba chetu yawapasa wasilalamike. Zaidi waitumie km part of learning

Exactly

Hawa wakiambuu ukitaka post kwa kiswahili kwenye majukwaa yao.

Wapambane na hali zao

Ha

Hapa tumepewa hifadhi Tu mkianza tena kuwachimba mtafukuzwa kama mbwa koko

Jana tu nilifurumushwa mkuu kwenye jukwaa moja Hivi

Wataanza kuiongelea lugha yako badala ya ulichopost.

Tuwaachie tu majukwaa yao huko, Sisi tuendelee na majukwaa yetu huku.

Tutaonekana sio waung’wana.

Kabisa tushakirimiwa tuendelee na harakati zetu

Issue ni kivumiliana, having an open mind and learning from each other. No one has exclusive rights to any language and we must appreciate that all languages are dynamic and take variations in different regions.

Sawaaaaa

kweli kabisa ukomavu ni kuvumiliana pamoja na kujifunza kutoka kwa kila mmoja wa wanakijiji.