Nimeiona hii title kwenye taarifa ya habari ya ITV, labda wenzangu mnisaidie , maneno kama hayo kutoka kwa Kadinali nafikiri si ya kubeza hata kidogo. Kwa jicho la tatu Kadinali kuna kitu amekiona which is something fish kwa ustawi wa catholic church and TZ as a whole, you are highly welcome for your contribution and views members!
Kitu gani amekiona kama si unafiki.Kwa mfumo wa kanisa Katoliki Askofu hana nafasi iwayo yoyote ile kuleta ukabila. Sema kama anatumia Propaganda za ki-CCM hapo tutaelewa.
Si amshauri swahiba wake Jiwe dhambi ya ubaguzi wa kikanda na ukabila anaifanya waziwazi?
Tatizo CCM walimtumia kuwapumbaza watanzania kwamba yeye ndiye Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania badala ya Rais wa Baraza la Maaskofu. Gwajima alipomnanga ndipo akaanza kuishi kama mchochea kuni kwenye kibanda cha gongo!
Huyu ametumwa aje kujibu hoja za Ruaichi.
Hana lololote unafki tu unamsumbua
Weka clip
Siku zote na mimi nilikuwa naamini jamaa ana power sana kumbe mamlaka yake ni ndani ya Dar tu.
Hana tofauti na Maaskofu wenzake wa Kanisa Katoliki. Ila CCM walikua wanamfanya kama yeye ni mtu mkubwa sana chini kidogo ya Papa. Kumbe Balozi wa Vatican ndiye bosi wa Kanisa hilo hapa Tanzania na ndiye kiungo kati ya Papa na Kanisa Katoliki Tanzania.
Pengo hana chake apambane tu na hali yake!
Halafu naye alijua ccm/serekali hawana ufahamu wa hilo akaitumia hiyo fursa kujikweza. Ukweli ulipowekwa wazi kwamba sio wa hivyo akawa na husda baada ya kushushwa. Bora atoke kwenye hiyo post akakitumikie chama kama akina judge Ramadhani na wastaafu wengine wa majeshi waliojitokeza waziwazi.
Na ndipo uone uwezo mdogo walio nao CCM!!
Hii yote sababu tunaongozwa na kiongozi mwenzake upeo mdogo na siye na kipawa cha uongozi
Hilo tu ndio kaliona. Mzee kazeeka vibaya sna
Aliwageuka maccm walotoa kijarida kulihusisha kanisa katoliki na ukabila katika TEC, amewaambia wasiogope kutaja makabila yao maana hawatumikii makanisa bali wanamtumikia yesu kristu.ccm yamebaki yatima ndani ya TEC maana swahiba pengo hatakuwa msemaji wao tena ndani ya TEC
:D:D
Sikilizeni maneno yake ya busara hayo
Pengo amekuwa akitumika sana,kwa awamu tofauti za uongozi hapa nchini
Sio wa kusikiliza tena huyu kashachoka, apumzike tu, na pia angeanzia mbali kukemea ukabila na ukanda katika awamu hii, nafikiri angeeleweka kuliko anavyotumika kwa sasa
Jamaa hazina kaweka hadi mtoto wa dada…hatari sana mkuu
Inabidi mshipa wa aibu uwe umekatika ndo unaweza kufanya teuzi za vile, hata kujishtukia hakuna!!!