Azimio La Arusha (1967) ni tamko rasmi la Serikali kuhusu Nchi itakavyoendeshwa kwa kutumia siasa ya ujamaa.na kujitegemea.
Kila mpenda usawa,haki, maendeleo anapaswa kuunga mkono jitihada zinazofanya na Rais JPM ambazo ziko wazi hazihitaji nguvu ya ziada kuonekana.
Kwa nchi yetu ilipokua imefikia ilihitaji mtu mwenye nia ya dhati na moyo wa kizalendo na uadilifu mkubwa ili kuitoa ilipokua na kuisogeza mbele kimaendeleo.
Raisi Magufuli imeonekana kuwa serikali yake inaenda sawia na azimio la ambalo lilikua na sehemu tano ikiwa ni,1.Itikadi ya chama cha Tanu, 2.siasa ya ujamaa, 3.siasa ya kujitegemea, 4.uanachama wa TANU na 5.Azimio la Arusha
Na kwa mwananchi anayejua yaliyomo katika azimio hilo ni wazi kuwa angependa kuongozwa na kiongozi anayeweza kuliishi pamoja na misingi yake.
Serikali ya Raisi Magufuli imeonyesha baadhi ya vitendo vilivyo ndani ya Azimio hilo ikiwepo,
Mapambano ya vita vya kiuchumi ikiwa ni moja ya ahadi alizotoa wakati wa kampeni zake za Urais mwaka 2015.
Mwalimu Nyerere alisema katika mapambano ya vita vya kiuchumi Mwalimu Nyerere alisema “Tumeonewa kiasi cha kutosha, Tumenyonywa kiasi cha kutosha na Tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndiyo uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka Mapinduzi, mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe, tusinyonywe tena wala tusipuuzwe tena”.
Na hiki ndicho Rais Magufuli amekua akikifanya mara kwa mara kupigania uchumi wetu ili tusioendelee kunyonywa
Pia tatizo la ufisadi Rais Magufuli amelishughulikia ipasavyo ambapo imeanzishwa mahakama ya mafisadi kwa ajili ya kushughulikia wabadhilifu wa uchumi
Pia fursa ya Elimu Bure ni kitu kilichodhihirisha namna Rais Magufuli anavyo tembea na Azimio la Arusha, ambapo azimio lilisisitiza kuwa maarifa ni nyenzo ya pili ya maendeleo yakitumika sambamba na juhudi. kwa kutambua hilo Serikali imetoa fursa kwa kuwawezesha watanzania maskini kupata elimu bure kuanzia Elimu ya Awali hadi kidato cha nne.
Ulipaji wa kodi, ni kati ya vipaumbele vinavyosisitizwa na serikali ya Dk. JPM juu ya kila Raia anayestahili kulipa kodi kufanya hivyo kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Na matumizi ya lugha yetu ya Kiswahili. ni kipaumbele ambacho Raisi Magufuli anaonyesha dhahiri dhana ya kuenenda na Azimio la Arusha. Ambapo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Baraza la kiswahili la Taifa (BAKITA) nao hawako nyuma katika hili la kuchochea matumizi ya Kiswahili kwenye nyenzo ya kuunganisha watanzania na kueneza Kimataifa.