Forex ama wengine hufupisha kwa kusema FX ni kufupi cha maneno Foreign Currency Exchange. Basically Ni biashara inayosisha kuuza na kununua fedha za kigeni. (Najua wengi hapa akili imegonga kwenye bureau exchange). Yes! Ni kitu kile kile lkn sasa hii Forex ni baba lao, tuwashukuru sana (wazungu) walioleta technology ya computer na Internet. Sasa kiuhalisia tukizungumzia Forex trading ni kubadilisha fedha za kigeni electronically and at real time. (Sijui kama unanielewa?). Ni wewe na computer ama smartphone yako pamoja na bundle lako.
Kinachotokea ni kwamba unaspeculate utendaji ama tuseme performance ya fedha fulani labda Dollar ama Yen ama Pound kisha ukifahamu uelekeo wake either utainunua ama kuiuza, kupitia huo mzunguko utatengemeza pesa kubwa sana ama kama ukijichanganya unapoteza vile vile. Hapa unahitaji uwe na uelewa mpana sana wa kufanya analysis ya soko la dunia (global currency market).
Hii ndio biashara yenye utajiri mkubwa kuliko biashara yoyote ile hapa duniani. Huwezi kuamini kwa siku katika forex trading kuna mzunguko wa $5 trillion (dola trillion tano), naomba hapa tusiiweke in Tsh maana tutaishia kuongea herufi za ajabu mara hexa trillion mara hepta trillion, lkn ni mkwanja mrefu sana. Kiasi kwamba itaihitaji New York Stock Exchange ifanye biashara siku 30 ili kupata pesa za siku 1 zilizopo kwenye forex market. Ndio maana sisi traders hua tunasema “kudownload pesa” yani kwenye forex ni kupakua tu pesa, kama vile upo uTorrent
Central banks zote zinafanya forex trading, financial institutions karibia zote duniani zinafanya forex, wafanyabiashara wakubwa karibu wote wanafanya forex (tena huyu bilionea wetu ambae alibahatika kufanya kazi Wall street atakua ni trader mzuri sana wa forex na stock), Donald Trump ndio hata usimzungumzie - huyu kashindikana, leo hii trump anasukuma tweets ambazo zinabadilisha upepo wa dollar katika soko ili yeye na team yake wagonge pesa, mpk anatoka madarakani atakua kazidisha utajiri wake hata mara 5.
Ukweli uliofichwa kuhusu forex
Sijui nisemaje, lkn ukweli ni kwamba kuna nguvu kubwa sana sana sana inatumika na mabenki kuwafanya watu wasiitambue forex. Wenzetu Ulaya na Marekani walishtuka mapema sana, kwao forex si kitu kipya sana japo bado kuna wingu kubwa hapo kati. Huku Afrika ndio usiseme, wenzetu SA kidogo wamewahi kushtuka kutokana na muingiliano mkubwa kati yao na mataifa ya Magharibi.
Utamu upo hivi - Leo hii ukichukua mil 10 na kuiweka benki katika fixed account, utapewa interest ya 7-10% kwa mwaka, hiyo miezi yote 12 unasubiria milioni 1. Lakini kwa forex ukiwa unajitambua ukaweka mil10 ukatrade, kama ww ni average trader ndani ya siku 2 utakua umepiga faida ya milioni 1. Sasa hapa benki zinapambana juu chini ili watu wasitambue forex ili wasije kupoteza wateja wa fixed accounts. Na ukweli ni kwamba pesa zinazowekwa fixed account bank hua wanazitumia kufanya forex trading, hii kuwapa watu mikopo hua ni kiini macho tu.
Hakuna bank yoyote ingependa ujue kuhusu forex, yani hata humo kwenye mabenki wafanyakazi wa humo humo benki hawatambui kabisa kuhusu forex. Ni wajanja tu ndio wanaweza wakaelewa nini kinaendelea huko duniani. Nguvu inayotumika si ya nchi hii.
Yani kuna blah blah vibaya mno, watu hawataki kufunguka kabisa. Lakini tutafika tu, dunia haiwezi ikatuacha just kwasababu ya manufaa ya wachache, sio fair.