Wakuu, najua kwa sasa angalau tunafurahia kujumuika tena huku uveneini. Sasa napenda kuuliza kuwa, jf yetu ikirudi hili jukwaa la huku litaondolewa au litabaki?
Tutajua mbele kwa mbele
Litabaki kwa matumizi ya baadae tena
Mzee baba…umemuita le mutuz:D:D
Itakuwa ndiko mabomu yanawekwa halafu Kule utaambiwa tu …aisee jf ya ktalk mambo ni faya…hapo ujue mafaili yashashushwa ni nyie tu kwenda kupakua.
Lakini vipi haiwezi leta mgogoro na jf yenyewe? Maana hata mpanhilio wa majukwaa na kama jf…? Ila kwa kiasi fulani nimeamini jf ni watu wenyewe
Hili litabaki kama akiba. Kumbuka kuwa JF yetu hukumbwa na misukosuko nyakati ya matukio fulani. Pindi yatokeapo matatizo kama hayo, JF ya hapa Kenya talk itakuwa kimbilio.
Ni kweli…hapo umenena.
Sidhani kama kutakuwa na shida kwani huku ni subforum tu ipo kama kule jftz kulivyo na Kenya forum na Uganda forum.
yaa hata mimi nashauri hili libaki kwa matumizi ya baadae
A
Amina
Tutaliweka kama akiba(mchepuko)
Yes, hii jf ya huku hatuwezi kuiacha bali itatumika kama recovery site pindi mambo yanapoenda ndivyo sivyo huku kwetu…!!
Litakuwa kama lilivyokuwa kabla ya sisi kufika. Hivi katika kambi ya wakimbizi kama wakimbizi wakirudi makwao inakuwaje?
Ni sawa na kuwa na nyumba mbili, hakuna shida
Litabaki liwe la dharura. Huwezi jua likirudi litafungwa lini tena.
Habari Mkimbizi mwenzangu…
Nyumba walizojengewa hazibomolewi, zinabadilishwa matumizi.
Ngoja kwanza irudi halafu tutajua cha kufanya…
Itaeleweka tu.