JF tunaomba angalau mtupe huduma ya "READ ONLY HASA KWA FORUMS KAMA....." kuna baadhi ya material tunahtaj sana sana zaid ya kuandika nyuzi

Kama mpo hapa na hilo likawa linawezekana kwa namna mjuayo tunaomb kwa kpnd hk mkiwa mnashughulikia kurud hewan kwa huduma zote basi angalau muachie zile nondo hasa forums za biashara uchumi na ujasiriamali, uvuvi mifugo na kilimo, matangazo madogo madogo, technique and technology . Huko kwenye siasa, MMU hata mkizifuta kwangu mimi sihtaj kitu labda kwa wadau wengne.

kwa ufupi Kuna vitu nahtaj mfan mashne ya popcorn, photocopy na salun kwa ujumla, kuanzia gharama za ununuz, uendeshaji, changamoto mbali mbali kwa wazoefu, mbinu na ushauri kutoka kwa wadau wenye uzoefu vitu ambavyo vyote vpo jf hata ukigoogle unaona kbsa unaishia kutoa udenda mana ukifungua unakutana na lile lijinotisi (hakuna maandish yananikera kama yale skuhz). Kuna fursa nimeziona/pata nataka nianze na ya popcorn kwa mwenye ujuz wa hii mambo naomb msaada.

kitu kingne naomb kuulizia, kuna vile vijitorori flan iv vipo sana dar, vinakua vya kuhfadhia na kutembezea vitu vdg vdg hasa vya kula na zaid hua bits na juice, kinaweza kiwe kimezungushiawa kioo au laa jina lake halisi sijui ila natumai kwa anayevifaham amevielewa, navipataje? Je kwa mkoani naweza kuvisafrisha? Gharama yake ikoje, naweza pata picha tofaut tofaut hapa nichague?
Amin hata upewe kila kitu ugenini nyumbn utapakumbuka tu, hakuna neno nikiliona linanikera kama “wakimbizi na ile notis ya jf” .

leo nimekua serious kdg mana weng wamenizoea kwa utani, ila hili limeniuma sana.
from live long jf to rise again jf? Poor me…

Hilo nahisi haliwezekani mkuu, hawawezi wakarudi nusu nusu.

Ila kiukweli hakuna jukwaa lenye madini kama jukwaa la Kilimo na Ufugaji, Biashara na Uchumi na jukwaa la Tec na education.

Yaliyobaki yalikuwa ni Furahisha Baraza tu.

Umesema ukweli, kuna Madini flan mule post za 2009-2013. Huwa zinaendelezwa tu na member wapya. Yafanyike yote lkn zile rejea muhimu kupatikana

Naunga mkono hoja!

mimi na jamii intelligence tu jamani

Naunga mkono hoja. Kama tatizo ni mzee chogolee basi jukwaa la siasa walizuie kwanza lakini majukwaa mengine kweli watuluhusu tusome tu

Watu wengi sana jamii media imewasaidia ikiwemo Mimi binafsi Kwenye jukwaa la afya Kuna dogo alikua anasumbuliwa na kifua nikaomba msaada Hakika nilifanikiwa kupata maelekezo sahihi na kutatua Tatizo. Kuiondoa hewani kumewanyima fursa Kubwa sana watanzania ya kujifunza na kufuatilia habari kwa ujumla

Umesahau jukwaa langu pendwa la intelligence

Lile jukwaa bwana nilikuwa nafurahi kusoma comment, mpaka comments zingine nilikuwa nasave.
Unakutana na comment za kina kiranga, Izzo, Eiyer, Malcom Lumumba, pundit, Mseza Mkulu, Zitto Jr, n.k.

Hakika lilikuwa limejaa maarifa.

Ninacholipendea jukwaa lile ni namna lilivyo fikirishi! Watu wanafikiri sana kabla ya kuandika

Hawawezi kuchia hata kwa read only… kinachohofiwa ni content au maudhui ya kule kuwa copy pasted na kupostiwa sehemu mbali mbali kwa sasa ambapo wana mashauri yao bado yanafanyiwa kazi…

Cc: @Mahondaw

Hakika mkuu maana kule ndani kuna madini mengi sana yamepotea

Jukwaa la Siasa ndani ya Jamiiforums ndio lililosababisha serikali kutunga sheria kandamizi kabisa ya Uhuru wa kufikiri iitwayo Kanuni za Maidhui Mtandaoni 2018, hizi kanuni zimeathiri wengi sana hata wasiohusika

Kweli waafrika mungu atusaidie tu ila wengi wetu ni wabinafsi sana.
Hivi INAMAANA VIONGOZI WETU HAWAJUI KUA KUNA MAJUKWAA YALIKUA YANASAIDIA WATU IDEA ZA KUJIKWAMUA NA UMASIKINI??.

Kweli aliyenacho hawezi kumkumbuka asiyenacho.

Jukwaa la siasa litakuwa hili huku KT…ila wangebakisha yale ya umuhimu zaidi kama wadau walivyotaja hapo juu

jf ilikuwa kimbilio LA wengi ilA washAmba hawajui umubimu wake

pengne ni kwa ajili ya maombi kama haya na mengne naona wametupa huduma ya READ ONLY ni hatua nzur kwa kweli