Wasalam.
Kama muhanga wa kusitishwa kwa huduma za JF, nimewaza na kuwazua bila kupata majibu. Wataalamu wa haya masuala mnaweza kutusaidia kama kuna uwezekano tupate forum yetu kuliko hili la kumezwa na KT.
Labda kama ungekuwa unamaanisha JF ihamishwe,na content zote tokea 2006 ziwepo…ila kama unamaanisha forum mpya mbona zimeshafunguliwa kibao tu…
Inawezekana endapo hiyo jf diaspora itakuwa subset ya hiyo forum kama ilivyo hapa ktalk
Kwa Sasa Ni ngumu kuaminika
Nakuunga mkono, Forum yoyote inayoanzishwa sasahivi iwe nje au ndani sio ya kuingia kichwakichwa.
Inawezekana JF wakaaungana ama kununuliwa ughaibuni,hofu yangu katika kipindi hiki cha mpito kina Melo wanapata tabu sana na huenda wakafika bei.JF ikawa chini ya wahariri Uhuru na mzalendo.Tuwaombee kina Melo,ikibidi kuwawezesha kifedha.
Wengine watachukua majina ya watu maarufu kule Jf na kujiita mwisho wa Siku anakamatwa kwa kosa ambalo lilitendwa na mwenye ID husika
Acheni kumuona jamaa ni cheap kiasi hicho kama kutuuza angekuwa alishatuuza toka kitambo tangu anaanza kupata misukosuko kwa ajili yetu.
Kuihamisha JF nje ya nchi bado itakuwa usumbufu kwa Melo maana bado atakuwa nchini
Hizo forum za kuanzishwa kipindi hiki cha JF kutokua hewani watu wanakua na mashaka nazo sana… inakua pia ngumu kuwaaminisha watu unaanzisha kwa nia njema…
JF imejijengea strong base of trust siyo kwa siku mmoja kwa kipindi kirefu sana…
Kule chochote husemwa, lolote hufanywa, makaburi kufukiliwa, mapovu kushushiana, BAN kutembezwa na maisha yanaendelea kwa amani kabisa…
Cc: @Mahondaw
Nahisi inawezekana
JF ndio wanaweza…
Yaah!! Na nibora wafanye hivyo
Na Wasitumie nguvu kubwa kuaminisha uma eti Kuna mbadala wa JF kwa sasa. Watulie tu Jf ipo kwenye Nyoyo zetu!!
Exactly