Ma dada ni kweli hakuna anaependa kuitwa maharage ya Mbeya maji mara moja. Lakini angalia upepo kwanza na majibu unayotoa.
Mkaka anakutokea unamwambia mimi nina mtu wangu, kumbe wala mtu huna, ulitegemea atafanya uchunguzi kwanza ndiyo agundue kuwa unamdanganya. Wengine hawapendi matatizo na watu wanaamua kutafuta aliye single anaendelea na safari.
Baada ya muda ameoa na imetokea mnaishi mtaa mmoja, tena wewe una grocery pale mtaani. Kumbe bado una fundo moyoni hata mkewe akija kununua mahitaji humchekei.
Wengine wanajibu mimi siko tayari kuwa na mpenzi sasa hivi. Mmh mwanaume akiacha kumtafuta baada ya mwezi anaanza kumtafuta kwa simu na kuuliizia habari zake kwa watu.
Msikilize jamaa atakavyopresent hoja zake. Kama huna jibu mwambie nipe muda. Kama unaamini Mungu, ukifika nyumbani liweke kwenye maombi Mungu atakuingoza. Kama una watu wa karibu unaowaamini unaweza kuomba ushauri.
Usikurupuke pia tunapenda kuona mnaiendeleza dunia.
Wasipoelewa na hapa hatuna kingine cha kuwasaidia.
Tatizo wadada wakiona kuna at least watu 4 wanamtongoza ndio nyodo huwa nyingiiiiii baadae yanakuwa yae ya Mchagua Nazi…