Jamiiforums siyo tena sehemu ya Kuonge kwa Uwazi na Uhuru. Dhana ya “Where we Dare to Talk Openly” haipo
Mkuu nini kimekukumba kule?.maana zama hizi ni vitisho mwisho mwisho
dead men tell no tales
Embu dadavua kuna nn kimekukumba
Yapo ya siri wanayoyatekeleza baada ya kurudi hewani na hatuwezi kuelezwa
Kule sina hata wazo la kurudi huko, hata app nilifuta kabisaaa
Tuko pamoja lkn tunakosa vingi sometimes ingawa kweli sasa hivi ni hovyoest ever
Mmmhh
Jirani urudi bana tunapata hata habari za MMU tu.
Mimi ninapotumi hizi App za KT na JF nakuwa kotekote. Kila nikipata notification upande fulani naenda kuiangalia na kuona kilichojiri
Nami ninazo zote mili ziko on full time
Pamoja sana mkuu
Najua siwezi kosa mengi kama jf ya hapo kabla! Serikali ikishakubana huna ujanja! Acha nibaki huku tuu
Jf nilikuwa nasoma majukwaa karibu yoote siasani ndo nilikuwa nasoma saaana! MMU pekee haitoshi wacha nibaki huku tuu labda miaka ijayo ila kwa sasa sina hata hamu na jf kabisaaa
Sawa jirani
ni kusoma tu sasa…
Mimi huwa nakwenda kule kuchungulia kisha natoka na kuja huku…
Mie Nachungulia sana kule ila watu wako na hofu kujilipua kama zamani
Mambo yameharibika tayari kule.
naona kama hivyo
Sasa ivi. Hali imekuwa ya kanyaga twende tuuu