Jamiiforum ya sasa hatari kwa usalama

Hivi katiba yetu Si inasema kila raia ana uhuru wa kutoa maoni na kuzungumza???

Sasa likes kwa post za nyuma hata haifai…
Wazee wa PM kumbe huko mko sana tu.

Ndio,ila ipo katika maandishi.

Hata wakiitoa tutabaki hukuhuku.

Mi sirudi huko ng’o!

Huko mi ntakuwa ndg msomaji tu

Kwani tatizo ni jina jf?au jukwaa huru?hata kama atawaambia kt waondoe jf,wakaanzisha jina jingine tu mf.jukwaa la watanzania bado litakuwa maarufu tu na jf original itakufa tu natural death,kama wakirudi kwa kukubali mapendekezo ya tcra!!watu hawafuati jina bali jukwaa huru na lenye kuweza kutunza siri za watumiaji wake!! Na hata jf ikirudi bado kuaminika tena itachukua muda kwani kuna maneno mengi yanasemwa!!!

bado anapewa masharti

Mi milipigwaga ban kabla haijafungwa, nimerudi kule kucheki bado ni maruweruwe tu…

Sasa Ni Nini maana yake Kama haifuatwi ilhali imeandikwa ili itimizwe

ndo maana tumewaomba mods wa kenya talk waanzishe BONGO FORUM AU TANZANIAN FORUM

Huwezi kujua mahusiano ya viongozi wa KT na JF yakoje, na hadi JF inaanzishwa humu walikubaliana vipi.
Lolote linawezekana.

Kama yule jamaa wa vkontakte alivyomuuzia putin ile website . Akahama nchi anaenda kuanzisha telegram

Kama kweli wananunua wabunge Wanashindwa vipi kuinunua jf? Na siajabu ishanunuliwa wanafundishana tu huko jinsi ya kuitumia.

Hekima na busara ni kuwa uhuru wa mawazo kwa nchi yetu chini ya Magu haupo kabisa, kwa sababu katiba imening’inizwa. Kwa hiyo ye yote anaetaka kushiriki kwenye JF yetu pendwa ajue JF kwa sasa ni chambo cha uhuru wa mawazo. Mimi nitaendelea kujitandaza humu.

Kisheria JamiiForums na Jamii Forums ni vitu viwili tofauti nielewavyo mimi. Kwa hiyo Melo atakuwa kimeo kama atathubutu kuhoji subforum hii ya Jamii Forums. Kwa sababu haziwi registerd NIDA ambapo majina yanalinganishwa. Kitaaluma ya komputa characters (word length) ya hayo majina no tofauti.

Angalia preveledges zilizoondolewa kwenye JF inatia wasiwasi kuwa sasa waendeshaji wana maudhui na madhumuni tofauti. JF is now a place where you do not dare to express your ideas.

Mimi sitarudi tena utumwani

Kama melo ndo kakubali,basiii tena li jf lao

Asante mkuu kuna kitu umenifungua

Utumwani tukafanyeje tenaa

jiwe limefanikiwa kuiteka tanzania yote
jf si salama nawaambieni