Itachukua Miezi mingi wana Jf wengine kujua kama tupo huku.

Salaam!.

Kusitisha huduma kwa Jf kumetufanya wengi kupata msongo wa Mawazo, mana ilikuwa ni sehemu nzuri yakutumia Bando kihalali, (Unaelimika).

Kwasasa tumehamia hapa kwa Majirani zetu Kenya, lakini hofu yangu nikwamba members wenzetu wengi tutawapoteza kwakutojua kuwa tupo huku.

Naona itachukua muda mrefu kuifanya jf kuwa na nguvu kama ile ya mwanzo.

Kila mtu awaaambie tushaanza kuja kuja huku

Ndio hivyo villager mwenzangu.

Hahahahaha nakuona new villager

Hatari kwelii, tutanyooka nau villager wetu, tumekuwa ma diaspora ghafla lakini

Huku unakujaje na id yako ya kule jf

Tunashukuru hawa ndugu zetu wametu accommodate kwa muda

sikujua km kuna siku ntakua mkimbizi wa fikra kaah

Ugeninini penye wenyeji wengi.

Msihofu vijana tushahamia uku tayari na wengine wanakuja

Mimi naamini itachukua siku chache sana watu kujua huduma ilipo na hasa kama juhudi za wapenda mabadiliko zitaunganishwa. Kama inavyofanywa na gazette hili.[ATTACH=full]175809[/ATTACH]

jamani mbona silioni jukwaa la wakubwa…jukwaa langu pendwa hili

Watu wakuja wengi hapa na maisha yataendelea

Watakuja tu taarifa zinaenea

Mkuu wengi walio addicted na JF utawaona huku soon kwani watu walikuwa hawana raha kabisa, kutwa unafungua website unakutana na bango, leo nimejaribu na baada ya bango nikafungua Gazeti la Mwananchi mara nakutana na Maxence akisema fursa imenyakuliwa na…Kenya talk…sasa hivi najimwaga bila taabu. Nabaki na swali moja kuu Server ya hawa wakenya ni kama ya JF?

Nami nmepata taarifa nimewasili kenya. Tatizo nmeshidwa kutumia login za jf ikabid njisajili upya

Kuwa mpolee uje taratibu upo ugeni i

Yaan mimi kweli nimekuwa villager mimiiii cc @Shunie

Si unaandika jina lako tu lile mbona sie tumeandika yale yalee

Mrembo wangu @Shunie upo na huku