Investment News: The Tanzania Investment Center (TIC) is participating in the Summit of Heads of State - FOCAC China

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinashiriki Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (Forum on China-Africa Cooperation - FOCAC) ulioanza tarehe 4 hadi 7 Septemba 2024 Jijini Beijing, China.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu unaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Miongoni mwa washiriki ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, TIC imewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji, Gilead Teri, na Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa Nje, Daudi Riganda.

Katika mkutano huu, TIC imeweza kushiriki katika matukio muhimu yafuatayo:
Kukutana na kufanya mazungumzo na makampuni kadhaa ya Kichina yenye nia ya kuwekeza katika sekta kama vile nishati, viwanda, utalii, kilimo, na ujenzi wa majengo (real estate).

Kushiriki tukio la kutia saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika kuhamasisha na kuvutia uwekezaji kati ya TIC na Weihai Municipal kutoka Jimbo la Shandong, China.

Kushiriki katika Hafla ya Chakula cha Jioni kilichoandaliwa kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji nchini Tanzania, ambapo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.

Kwa siku ya leo, TIC itakutana na Watanzania wanaoishi China (Diaspora), ambapo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atakutana na kuzungumza nao.

https://x.com/InvestTanzania/status/1831928768929161286

Wapi nudes za suluhu

Hawataki News zangu