Ikulu inahusika na huu ufisadi?

[SIZE=7]Kamati ya Bunge yabaini kashfa katika stempu za kieletroniki[/SIZE]

http://sautikubwa.org/wp-content/uploads/2018/04/MdAoZ-7p_400x400-150x150.jpg
[U]Ansbert Ngurumo[/U]
Posted on [U]19th June 201820th June 2018[/U]

Kamati ya Bajeti imesema Stempu za Kielectroniki (Electronic Tax Stamp-ETS) NI KASHFA KUBWA: [COLOR=rgb(226, 80, 65)]Kampuni iliyopatikana kinyemela kulipwa TZS67 bilioni kwa mwaka. Hii hapa kauli ya kamati kama ilivyowasilishwa na Hawa Ghasia.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2018/19 Serikali imedhamiria kuanzisha Mfumo wa Stempu za Kodi za Kieletroniki ili kudhibiti udanganyifu wa wazalishaji wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa. Kampuni ya SCIPA kutoka Uswiss ndiyo iliyoshinda zabuni hiyo hapa nchini na ina mkataba wa miaka mitano na Serikali kwa mfumo wa Self Financing. Mfumo huo unamtaka mwekezaji kurudisha gharama zake za uwekezaji kwa kutoza stampu ya kieletroniki kwa kila bidhaa itakayozalishwa. Kiasi cha fedha kinachotarajiwa kuwekezwa na SCIPA ni Dola za Marekeni 21,533,827 sawa na Shilingi 48,472,644,577.

Mheshimiwa Spika, Kamati haina pingamizi na uanzishwaji wa mfumo huu, jambo la msingi ambalo linahitaji lifanyike kwa umakini ni kujiridhisha na gharama za mfumo huo ambazo zitabebwa na watumiaji wa bidhaa pamoja na mapato atakayoyapata mwekezaji kutokana na stempu.
Mheshimiwa Spika, Kamati ina maoni kuwa hatua ya Serikali kutoongeza ushuru wa bidhaa zisizo za petroli itakuwa haina maana kama gharama ya stempu itabaki kama ilivyopangwa na Serikali. Hatua hii itasababisha kuongezeka kwa bei kwenye vinywaji kama maji, soda, bia na juisi ambazo sasa hazitozwi stempu. Aidha, tathmini ya Kamati inaonesha kuwa pale Serikali itakapokuwa inaongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia ya mfumuko wa bei kama Sheria ya Ushuru wa Bidhaa inavyotaka, kiwango cha stempu kitakuwa kinaongezwa juu yake kulingana na Mkataba kwa miaka mitano (Rejea Jedwali Na. 5 na 6) linaonesha jinsi bei itakavyoongezeka kwa vinywaji baridi.
Mheshimiwa Spika, Kamati imefanya uchambuzi ili kubaini kiwango cha fedha ambacho kampuni ya SCIPA itakipata katika Mkataba huo kwa Mwaka mmoja. Uchambuzi huo umehusisha takwimu za bidhaa tatu za maji, soda na sigara bila spiriti kwa kuangalia viwango vya uzalishaji wa bidhaa hizo kwa mwaka. Uzalishaji huo unaonesha Kama ifuatavyo:- kiwango kinachozalishwa nchini kwa mwaka; Maji ni lita za ujazo 268,702,209 Soda ni lita za Ujazo 732,315,008 Bia ni lita za ujazo 409,274,746 na Sigara ni Pakti 429,310,400.

Mheshimiwa Spika, ukikadiria kwamba stempu itatozwa kwa idadi (unit) na sio kwa ujazo (lita), hivyo chupa moja ya bia ml 500 itatozwa Shilingi 22.73; Soda 500 mls itatozwa Shilingi 13.5, Spirit 1000 mls itatozwa Shilingi 29.57. Hivyo, ukijumlisha na ushuru wa bidhaa kwa kila bidhaa iliyoainishwa hapo juu inaonekana kuwa gharama itakwenda kwa mlaji wa mwisho. Kwa mantiki hii, ukokotoaji unaonesha kwa mwaka mmoja SCIPA atakusanya jumla ya Shilingi 66,690,313,798.84 bila ya kuhusisha takwimu za bidhaa ya spiriti. Aidha, Kiasi hiki ni kikubwa kuliko alichowekeza katika kipindi cha mwaka mmoja tu wa mkataba.

Mheshimiwa Spika, Kamati imekuwa ikifuatilia hatua mbalimbali za Serikali zenye lengo la kukusanya mapato yake yenyewe na sio kutumia mawakala kukusanya mapato. Mfano; kuhamisha fedha zake kutoka Benki Binafsi kupeleka Benki kuu, mfumo wa manunuzi ya Luku kutoka Kampuni ya Max Malipo na Mitandao ya simu kwenda GePGS (Government Eletronic Payment Gateway Systerm), ukusanyaji wa mapato katika mabasi ya mwendo kasi na matumizi ya mashine za EFD.
Mheshimiwa Spika, Kamati inaona kuwa Serikali kuamua kumpa SCIPA Mkataba wa miaka mitano wa kuhakiki uzalishaji kupitia stempu za kielektroniki ilhali uhakiki huu ungeweza kufanywa na Serikali yenyewe. Hata hivyo, Kamati imeona kuwa kiwango cha mapato kinachotarajiwa kukusanywa katika kipindi cha mwaka mmoja (Shilingi 66,690,313,798.84) kwa bidhaa nne zilizo ainishwa hapo juu ni kikubwa kuliko kiwango cha uwekezaji cha Shilingi 48,472,644,577 ambacho kimewekezwa na Kampuni ya SCIPA. Baada ya Kamati kufanya uchambuzi huo inaishauri Serikali yafuatayo:-

i. Serikali iwekeze yenyewe mfumo huu wenye mtaji wa kiasi cha Shilingi 48,472,644,577 ili kiasi cha fedha kitakachopatikana iwe ni sehemu ya mapato ya Serikali badala ya mapato yatokanayo na stempu kuchukuliwa na Kampuni binafsi kama ilivyofanya kwenye Mfumo wa TANCIS;
ii. Serikali ianze kutumia mfumo huu kwenye vinywaji vikali ambavyo mara kwa mara mbele ya Kamati Serikali imekuwa ikithibitisha kuna udanganyifu mkubwa; na
iii. Ni bora Serikali kuongeza ushuru wa bidhaa kwa asilimia 5 ya mfumuko wa bei kama ilivyokuwa ikifanya hapo awali kuliko inavyopendekeza sasa kutumia mfumo wa stempu kwa bidhaa hizo kwa kuwa gharama za stempu ni kubwa kuliko ushuru wa bidhaa wa asilimia 5. Mathalani ukichukua bidhaa ya soda (250 ml) inatozwa ushuru wa bidhaa kiasi cha shilingi 15 na wa stempu utatozwa kiasi cha shilingi 13.5. Hivyo, gharama ya jumla (gharama ya ushuru wa bidhaa na wa stempu) itakuwa kiasi cha 28.5 na hivyo itaongeza gharama kwa uzalishaji na kwa mlaji.

Nimeuliza kama Ikulu inahusika maana kulikuwa na ufisadi mwingine wa kutisha fuatilia link hapa chini ambapo Ikulu ilihusika lakini hakuna chochote kilichofanywa na “mpambanaji wa ufisadi” pamoja na kuwepo mahakama ya ufisadi kaminya kimya kimya bila hata ya kutoa neno hata moja.

http://www.jamhurimedia.co.tz/serikali-ichunguze-e-passport/

Pia kama mtakumbuka shilingi 1.5 trillion ambazo hazijulikani zilipo huyo kubwa la majizi hakuona umuhimu wa kuunda tume ya kuchunguza kilichotokea kuhusiana na pesa hizo kwa sababi yeye na genge lake la wahuni wanahusika na upotevu wa pesa hizo, vinginevyo mtu anayeijali nchi yake hawezi kukaa kimya kuhusu upotevu wa 1.5 trillion.

Huyu jamaa anaiingiza nchi hasara kubwa sana kwa kigezo cha uzalendo…na ndio maana anatumia nguvu kubwa sana kutunyamazisha wananchi ili tusiongilee ufisadi wake.

Serikali kimyaaaa hakuna uchunguzi $57 millions sawa na 90 billions zimepigwa na sasa bilioni 67 zimepigwa tena jumla 157 billions mafisadi wa Ikulu wamefanya yao. Na “mpambanaji wa ufisadi” kauchuna tu WE ARE ON LAITI TLAK isomeke we’re on the right track! Seriously???

Nakuona Mkuu sasa unaona janga kubwa la huyu dikteta. Huyu ndiye yule Idawa ambaye niliamua kumfollow miaka ya nyuma kwa kuwa kila alichoandika kuhusu hatima ya nchi yetu tulikuwa on the same page.

Hadi wewe Idawa umeona hii?

Jamaa haendagi nje kuna wana ni makuwadi wa upigaji

!
!
Tutembee Vifua Mbereee. Tuko On The Right Truck And Road To Hell

Halafu unakisikia kikisema eti kinapambana na ufisadi. Hovyo kabisa.

Mkuu huyu ndie MWIZI no 1 kwa hivi sasa.
Hana lolote la kupambana na ufisadi wala nini…
JIZI.

Hmm!.. :eek::eek::eek:

upigaji ni matokeo ya centralization, kila kitu kimehamia “ofisi ya rais” unategemea uwajibikaji hapo??? maana wao ndio wanajiona wasimamizi wa wengine na hakuna anayewasimamia hivyo wanajipigia tu kimyakimya, Bunge letu ni bure kabisa wanaishia kupiga soga tu hakuna kuiwajibisha serikali ndio maana imefika point hadi pesa za ushuru wa korosho zimepigwa

Alianza na epassport akaja trilioni 1.5 sasa hivi kapiga kwenye stamp. Uyu jamaa ni fisadi mkubwa sana.

Hee bwana, hii ya korosho nimesikia hasubuhi kwenye magazeti, inasikitisha kwakweli.

Deal hilo lingeweza pigwa na Kampuni ya Kitanzania Sema serikali hii ni kama haipendi kabisa mbongo awe na Hela. Kwanza najua huo mtaji wa 48bln umekuzwa sana ili hao waswisi wajustfy gharama zao.

Kubwa la majizi Mkuu

:mad::mad::mad:

Mkuu ile 1.5 trln aliulizwa CAG mbele ya kamera, tena Ikulu kama imepigwa au la…mambo yakaishia pale, akaibuka Chakubanga na hesabu za kipuuzi mchezo ukaishia pale. Ukweli taifa letu linapita katika wakati mgumu sana Mungu aingilie kati…kama kuna watu wanadhani tunaenda vizuri hao wanahitaji huruma ya Mungu tu

Duh

Nimeshamjua anaeturoga waTz