Ibara ya Katiba inayolifanya Bunge liwe mateka wa Serikali!

Ibara ya 67

(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo

(a)
ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
[SIZE=5]COLOR=rgb(184, 49, 47)[/SIZE]
[SIZE=5][COLOR=rgb(184, 49, 47)]ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na[/SIZE][SIZE=5][COLOR=rgb(184, 49, 47)] chama cha siasa;[/SIZE]
(c)
katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika maha
kama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali. Mwisho wa kunukuu.

Utepevu wa Bunge letu unatokana na kipengere hicho cha “b” kwenye katiba yetu. Maana yake ni kwamba vyama vya siasa vimepewa madaraka makubwa sana dhidi ya wabunge kuliko wanainchi waliowachagua. Mbunge wa chama tawala ama upinzani anayetaka kupingana na chama chake ni lazima awe na hakika kwamba akifukuzwa uanachama, basi anaweza kurudi tena bungeni kupitia chama kingine.

Sasa kwa hali halisi ni nani anayeweza kuhatarisha ubunge wake eti kwa kupingana na serikali ya chama chake wakati anajua kwamba Rais ndiye pia Mwenyekiti wa Kamati Kuu ambayo inaweza kumnyang’anya uanachama na yeye kupoteza ubunge? Kama kipengere hicho kisingekuwepo wabunge wangekuwa huru kuipinga Bajeti na kupambana na serikali bungeni.

Suluhisho ni kuwa na kipengele cha mgombea binafsi

Wakisikia habari ya mgombea binafsi wanapata depression.Tangu enzi ya Mkapa; hadi wakapeleka mswaada bungeni haraka haraka (baada ya Mtikila kuwabwaga mahakamani) ili kuhalalisha kuzuia kuwepo wagombea binafsi

Siku katiba na sheria zetu zitaruhusu mgombea binafsi ndipo tutakuwa na bunge la wawakilishi wa wananchi kweli kweli

Leo hii wabunge karibia wote wa ccm huikosoa serikali kwa tahadhari sana ya kuwaudhi wenye chama ambao ndio hao hao wanaowakosoa walioko serikalini ambao wanaweza kumpora uanachama wake mbunge yeyote na kwa wakati wowote ule atokanaye na chama chao na automatically kupoteza sifa ya ubunge, hivyo sifa ya mbunge kuwa lazima atokane na chama cha siasa ni kansa inayolitafuna bunge letu leo, kesho na hata kesho kutwa kama hakutokuwapo mabadiliko hayo ya katiba yanayohalalisha mgombea binafsi

Ni wakati sasa kwa Watanzania wote pasipo kujali itikadi zetu zozote zile tupiganie mabadiliko hayo ya katiba ili tuwe na bunge la wawakilishi kweli wa wananchi siyo hili bunge la wezi, wachumia tumbo, majambazi, vibaka na kila aina ya upumbavu.

Magufuli kama kweli angekuwa na akili timamu kweli kweli za uchungu na mlala hoi was nchi hii hakika haya ni sehemu ya mambo muhimu sana angepaswa kuanza nayo, lakini kwa sababu ndio wale wale wazalendo hewa na majambazi ya rasilimali za nchi hii yaliyo tayari kumuua yeyote yule anayehatarisha ulaji wao binafsi tusitarajie mabadiliko chanya yoyote yale yaliyo na afya pana kwa maslahi ya nchi

Ukombozi wa fikra katika taifa hili hauko kwa wanasiasa kamwe, mwanasiasa mtaji wake mkubwa ni ujinga wa wananchi, maradhi, umasikini na ujinga ndio haswa unaliangamiza taifa hili.

Hicho kipengere kibadilishwe na kisomeke “ni mwachama wa chama cha siasa ama mgombea huru” na ikiwezekana kiongezewe kipengere kuzuia vyama vya siasa vikimfukuza mtu uanachama wa chama husika kupoteza ubunge ama udiwani. Cha ajabu Rais hajawekewa sharti hilo.

Toka nimsikie Taahira Kibajaj akiwapiga mkwara wabungewa CCM juzi nimehitimisha kwamba Tanzania haiwezi tena kupata chembe ya Maendeleo kwa CCM kuwa madarakani…
CCM ni kusanyiko la binadamu WAJINGAna WAPUMBAVU.

Hahahahaha hao wabunge jamii ya Lusinde ndio wapendwa wa bwana yule mpenda mapambio

!
!
Nadhani Tunaanza Kujua Maana Ya Mhimili Uliojichimbia Zaidi

ivi kuna mbunge anaweza ripa mil 500?kupitia biashara zake binafsi,km jibu ni HAPANA.bc sidhani km kuna wabunge wanaweza pingana na mamlaka aliyopewa jiwe.

Ni mtihani sana…

Cc: @Mahondaw

Mkuu wala hawamuogopi hata huyo mgombea binafsi. Hawakawii kutunga sheria itakayomfanya spika afute ubunge wa mbunge yoyote binafsi pindi asiporidhishwa na mwenendo wake. Na huko kwenye uchaguzi wa mgombea binafsi usishangae sheria zitakazotungwa zikiwafanya vibaraka kuchaguliwa.

Mfano wa hila za hao jamaa ni kama wajumbe wa bunge la katiba waliotoka kwenye makundi maalum mbali ya wabunge wa vyama. Bunge lile lilikuwa na tofauti gani na hili la ccm la sasa? Unakumbuka wajumbe kama viongozi wa dini walichokuwa wanaongea? Unakumbuka yule shehe mnafiki aliyeigiza kulia eti Lissu kamtukana baba wa Taifa!? Namna pekee inayoweza wangalau kuleta katiba kama ya Kenya ni machafuko.

Hicho kipengele ni moja ya vikwazo kwa maendeleo ya nchi yetu. Pia huwa tunakosa watu wazuri kuwa wawakilishi wetu kisa tu hawana influence kwenye haya mavyama ya siasa. Hiyo sheria inabidi ikapingwe tena mahakamani. Hiyo sheria moja ndiyo inayofanya CCM isimame mpaka leo. siku ikotoka na CCM itakufa.

kwakweli Tanzania hatuna bunge, Nyerere aliitumbukiza nchi kwenye mfumo wa hovyo sana wa kiutawala sijui hata kwanini watu wananing’iniza picha zake ofisini

Kwa kweli inasikitisha sana!

Tunapitia kipindi kigumu mno!
Nalog off

Nimekusikia katika Radio Ebony Mkuu upo njema sana kwa nondo zenye mashiko

Haya ni miongoni mwa maswala ambayo hayatakuja kurekebishwa kirahisi rahisi …

Kwa ivo nini kifanyike!!