How does covid kill: kiswahili mingi.

Nikisoma maujumbe mengine huku na huko ninaona watu kiasi ni kama hawana taarifa kamili covid 19 ni nini.

I will just put this here.

Hizi picha hazijatoka Kenya. Lakini ziko nyingi sana kama hizi tu hapa kwetu Kenya.

Mtu ambaye ameugua covid mara nyingine huja hospitali asijue ako na shida kubwa. Atakuwa na homa na anaumwa na kichwa na unaweza kupata kiwango cha hewa safi ya oxygen kimeshuka kidogo tu. Ukipiga picha ya kifua inaweza kuwa hivi kama hii ya kwanza hapa chini:
[ATTACH=full]357157[/ATTACH]
Ukiangalia hiyo picha ya kwanza unaweza kuona dhahiri vitawi vya mishipa ya damu (blood vessels) na vifereji vidogo vya hewa (bronchi) ambazo kwa pamoja husambaza oxygen mwilini. Baada ya kupimwa kwa kipimo cha antigen ambacho hurejesha matokeo papo hapo ukapata kumbe mgonjwa ana SARS CoV 2 (Covid 19). Mgonjwa anaweza kuwa hana tatizo kupumua lakini daktari kwa kuona ako na kisukari, ni mnene ako na uzito, na pia ni mgonjwa wa mkimbio wa damu akataka kumlaza. Mgonjwa akiwa anajiskia vizuri anaweza kuwa na upeketevu fulani hio akapewa dawa KUENDA NYUMBANI.

Kwa picha ya pili ambayo imetokea baada ya siku tatu, mgonjwa ametumia dawa nyumbani lakini hali yake ikawa mbaya. Utaona kwa hiyo picha mapavu yamepoteza muonekano wake wa kawaida. Vifereji vya hewa na pia mishipa ya damu haionekani vizuri. Huyu sasa kiwango cha oxygen kwa damu kinaweza kuwa kimeshuka kufikia 80% au chini zaidi.

Kwa picha ya tatu, siku ya sita, utaona kuwa hakuna tena uwezekano kuona mishipa ya damu wala vifereji vya hewa katika mapavu ya mgonjwa. Pia ukiangalia kwa makini utaweza kuona kuna nyaya na tube zimewekwa kupitisha lishe, dawa, hewa, na pia za kuweza kubaini (monitor) hali ya mgonjwa inayodorora. Huyu mgonjwa akikosa nafasi ICU atakuwa HDU.

Vita ambazo madaktari wanapigana huko ndani sio feki. Kunazo hatari za covid. Wengi hawajaona, kwa hio hawajali hata. Lakini covid si ugonjwa mzuri. Ni ugonjwa mbaya.

Kiswahili Mingi saidi

Sheng pls, hii hatuelewi

Kwani wewe ni Mtanzania?

I am using swa to try to bring this thing home. I think many guys I interact with think we are making a storm in a tea cup. If you get into a matatu, shop, restaurant etc, the guy next to you could be diabetic, hypertensive, could be older than you think, could be on immune suppressive treatment, asthmatic, or have some other chronic lung disease; na usijue. Please keep them at a distance. Dont breathe in to their face. Be considerate.

[ATTACH=full]357218[/ATTACH]

Kenyans dont need convincing. They are past that. This is a message best suited for Tanzanias. Especially now that its 99% in Chiswahiri

Unacheka nini boss?

Hio ndio gani?? Sijawai skia

:DWacha kutuenjoy wewe. You know what CoV is. Labda useme hujui CoV 1 na CoV 2 tofauti yake.

alafu @thesavage ulitumia kamusi ama we ni mnoma tu chiswahiri like that ?

Cha kuongea najua. Lakini sarufi kuchora mimi hupata sufuri. Nothing in that write up is worth a kamusi. Btw if you give that kapassage to a swahili teacher utapata sufuri. Swa nimeongea sana nikiwa mtoto manake nililelewa mwambao kuongea swa sina problems. But written swa for me ni zero.