Hivi, "Mbuzi wa Shughuli" Maanake Gani?

Nauskiza wimbo Utaipenda wa Hussein Machozi, na hapo inapoanza, anaimba, “mimi si mbuzi wa shughuli”.

Nisaidieni kidogo. Msemo huo unamaanisha nini? Kwa kweli, nitapenda kujua.

Ahsanteni.

https://www.youtube.com/watch?v=pV0VQA5b9pY

Nimegoogle, nimepata movie tu. Na link ya kwenda jamiiforums.com, ambayo kwa sasa imefungwa. Hata ninapotumia Web Archive ( http://web.archive.org/web/*/https://www.jamiiforums.com/threads/mbuzi-wa-shughuli.707709/ ) haipo.

[FONT=courier new]Maana yake ni Pumbu / Kende.[/FONT]

Mbuzi wa shuguli ni yule aliyeandaliwa maalumu kwa ajili ya kuchinjwa kwenye matukio mbalimbali kama Sherehe, kilio n.k

Ni kama kutolewa kafara fulani…

Mda wowote kisu.

Mbuzi wa shughuli mathalani NDAFU hupitia pilikapilika nyingi sana mfano kutolewa mazingira yake aliyokuwa ameyazoea na kupelekwa asikokujua tena akiwa na kamba shingoni sasa akikumbuka Kule alikotoka yeye ndiye alikuwa mbabe,mtawala wa majike kadhaa anajikuta akihangaika kutaka kukimbia saa zote huku pia hofu ya kisu ikimzidishia wasiwasi…sasa yeye Hussein machozi anasema hana wasiwasi kwani yeye siyo mbuzi wa shughuli akimaanisha kuwa hamhofii mkewe kwenda kutafuta chakula iwe sokoni au kufanya biashara yeye atajipumzisha tu home hana wasiwasi na mkewe,anamwamini…

Kwahii tafasiri nilioipata kwenye akiliyangu… Naomba nisiiweke kimaandishi hapa, maana tunaweza tumakimbiana… tehteehhh

Haya yanaitwa mawazo mabaya hahaha

Ni mbuzi ambae hufanyiwa yote mazuri kwa kile kipindi kifupi anachosubiria kwenda kuchinjwa na kugombaniwa kwenye sahani…

Cc: @Mahondaw

Ahsanteni.
Kwa kweli, wimbo huu una maana nyingi - iliyo wazi, na ile fiche.

anytime anachinjwa

Mbuzi wa machagadema huyo

Sawa karibu tena mkuu