Hii ni ya Wananchi Watukufu wa Pwani

FROM A CITIZEN #MOMBASA
DHULMA ZA KIHISTORIA ZA WAPWANI
Haya ni maoni yangu kuhusu hili swala , na mtazamo wangu ni huu.

Hili ni swala linalotajwa na wanasiasa katika majukwa ya kisiasa kila wakati wa kampeni za kisiasa.

Gavana Joho na mwenzake mbunge wa Mvita wamelishikilia sana hivi karibuni swala hili , kama wengi mumesikiya wakitaja maonevu ya wapwani ya kihistoria katika mikutano ya kisiasa.

Wapwani watakubaliana kuwa kuna mambo ni lazima yaangaliwe kwa makini na yasuluhishwe ili kuridhisha hisia za watu wa pwani. hapo nadhani sote twakubaliana.

Pahala ambapo wapwani tunajisahau kila hili swala linapotwaja katika majukwaa ya kisiasa haswa wakati za kampeni za kisiasa ni haya hapa chini.

Ripoti ya TJRC imekuwa tayari kutoka mwaka wa 2013 , lakini licha ya hili, inasikitisha kuwa wabunge walioko hivi sasa wamezembea kwa kutopiga kelele kutoka wakati huo wote kuitisha kuwa ripoti hii ijadiliwe bungeni. Hivi karibuni ambao sasa ni wakati wa kampeni swala hili wamelizusha tena.

Wanasiasa Wanao ongea kuhusu hizi dhulma za wapwani za kihistoria wamekuwa katika siasa miaka mingapi? tuchukue mifano.

Gavana Joho
Ameanza siasa mwaka wa 2004 , mpaka sasa mwaka wa 2016 ni miaka 12 katika siasa , ambapo amekuwa mbunge , amekuwa katika wizara tafauti tafauti na sasa ni gavana.

Sasa , sisi kama wapwani ni lazima tujiulize miaka yote kumi na mbili baada ya vyeo vote hivi ameshindwa kutatua haya mambo? ambayo kila wakati wa kampeni ukifika hua yafufuliwa upya ?

The Nassir’s
Hawa wamekuwa katika siasa takriban miaka 30, kama wabunge, na katika wizara tafauti na nyadhfa mbalimbali katika serikali ya KANU na ODM. Ukichanganya mzazi na mtoto.

Sasa , sisi kama wapwani ni lazima tujiulize miaka yote hii zaidi ya ishirini na tano baada ya vyeo vote hivi katika serikali wameshindwa kutatua haya mambo? ambayo kila wakati wa kampeni ukifika yanatwajwa??

Kwa mpwani mwenye akili yake timamu , Kiakili mtu akiangalia ataona wazi kuwa kuna kitu ambacho hakiko sawa. Wazungu wanasema - Things don’t add up and Numbers do not lie.

Sasa ikiwa miaka yote hii kuwa katika siasa na serikali wameshindwa kutatua na kuleta suluhisho , nikama sisi wapwani tuko katika duara , twaanza , kisha wakati wa kura ukifika twaregea palepale tena. Miaka yote hii na suluhisho wapwani hatuletewi na viongozi wetu , hatuoni kuwa kuna kitu ambacho hakiko sawa hapa?

Suluhisho ni lipi? Suluhisho ni kuwapa watu wapya fursa hizi za kuwa katika siasa na serikalini na wapwani kuwapa muhula maalum ya kutatua haya mambo. Ni lazima tujitoe katika hili duara na tuweke vipimo juu ya mambo haya katika huo muhula.

Na nilazima watatue haya mambo katika muhula wa miaka mitano pekee. Hao watu wapya wakiwa wamefanya kitu katika muhula huo wa miaka mitano basi tunaweza kama wapwani kuwapa tena kura ili waendele.

Lakini tukienda kiholela bila ya kutumia mambongo yetu , hili duara ambalo tumo ndani halitamalizika na hakuna natija tutaona , itakuwa twenda kama kondoo.

Sasa tuangalie serikali tafauti tafauti na vipi wamejitahidi kutatua swala hili.

KANU
Haikufanya jitihada za kushughulikia swala hili , licha ya kuwa wanasiasa wa Mombasa tuliowataja hapo awali walikuwa kwenye chama hichi kwa miaka zidi ya ishirini.

ODM
Waziri mkuu alikuwa ni Bwana Raila na waziri wa ardhi alikuwa ni James Orengo.
Na licha ya kuwa wanasiasa wa Mombasa kuwa katika chama hichi , swala hili halikutatuliwa na yakuskitisha Zaidi ni kuwa hati miliki za ardhi walizotoa kwa wapwani ni chache sana licha ya kuwa na uwezo wa kulishughulikia jambo hili kikamilifu.

JUBILEE
Mrengo huu ndio mrengo umetoa hati miliki za ardhi kwa wapwani nyingi kabisa katika histora ya Kenya , Zaidi ya Millioni 2,405,000.
Licha ya kuwa mrengo huu haukuwa na wanasiasa kama wabunge na magavana katika pwani.

Too much Kiswahili. @xuma come and do a summary please

Wapwani ni Waswahili, Mboss!

Yote Tisa, la kumi tupatie Uhuru Kura?

That is the conclusion of your article.

Mimi niitwe dual resident. Mwili iko Nairobi lakini roho iko Diani. Hata mkitaka nitachukua mdigo, nimkimbize kanisani kwanza ndio nijue kama labda ni mfwasi wa @jumabekavu ndio nianze kumfuga

nimesoma kiswahili mingi Leo kihiko niliosoma shuleni.

now i have headache, feel like throwing up, kuhara na baridi at the same time. Might be too much swahili.

Google Translation

FROM A CITIZEN #MOMBASA
violence History coastal
These are my views on this issue, and my view is this.

This is an issue mentioned by politicians in carousel political all during political campaigns.

Governor Joho and fellow MP Mvita had kept very recently this issue, as many mumesikiya citing abuses coast historic rallies.

beach you will agree that there are things it should be monitored carefully and yasuluhishwe to satisfy the feelings of the people of the coast. then I think all of us echo.

Pahala where the beach we forget all this query linapotwaja in political arenas, especially during the political campaigns are as below.

Report TJRC has been prepared from 2013, but in spite of this, it is sad that the MPs who are now have neglects not to shout from time to time to convene all be discussed in parliament this report.Recently now it’s time to have lizusha campaign this issue again.

Politicians Those who speak about these historical injustices coast have been in politics, how many years? take some examples.

Governor Joho
Started politics in 2004, so far in 2016 is 12 years in politics, where he has been a member of parliament, has been in the ministry different variations and is now governor.

Now, we like the beach we must ask ourselves all these years after twelve titles vote has been unable to solve these things? that every time you come hua campaign yafufuliwa reviewed?

The Nassir’s
Eve have been in politics almost 30 years, as legislators, and in different ministries and different government nyadhfa of KANU and ODM. Combined parent and child.

Now, we must ask ourselves if the beach is all these years more than twenty-five titles after this vote in the government failed to solve these things? that every time you come yanatwajwa ?? campaign

to shore with his faculties, Intellectual someone watching will see clearly that there is something that is wrong.Europeans say - Things do not add up and Numbers do not lie.

Now if all these years to be in politics and the government failed to resolve and bring a solution, somehow we beach we’re in a circle, we are beginning, then when the vote is reached twaregea stagnant again. All these years we letewi coast and solutions to our leaders, we feel that there is something is wrong here?

The solution is there? The solution is to give these people new opportunities to be in politics and government and beach give special semester to resolve these matters. We must present ourselves in this sphere and put measurements on these things in the same semester.

And they must to resolve these matters in a term of five years only. These new people as they have done something in the term of five years then we might as coastal give back the vote to go forward.

But we may arbitrarily without using mambongo us, this circle that we are in the wrap up with no conclusion we will see, it will twenda like sheep.

Now look at government different variations and how they strive to solve this issue.

KANU
Haikufanya efforts to address this issue, even though politicians in Mombasa we have mentioned previously were in this organization for years to exceed twenty.

ODM
prime minister was Lord Raila and lands minister was James Orengo.
and despite that politicians of Mombasa have in this organization, this issue is likutatuliwa and yakuskitisha More are being patented land they have made for the beach is very limited despite being able to deal with it effectively.

JUBILEE
wing this is the wing has issued a warrant possession of land to the beach quite a lot in history of Kenya, Over 2,405,000 Million.
Besides that this was not a wing politicians as legislators and governors at the beach.

kiswahili chako ni kizuri sana ndugu wachana ni hizi ghasia@byro na kadhalika hawa ni waacha mila. kwa swala la siasa jiunge na chama cha baba na mama (jubilee)
na mambo yatakua shwari,

Ahsante sana! Sikuandika mimi mwenyewe, lakini! Nimecopy kutoka Mombasa county government watch Facebook page.

WRONG! Wapwani wote si Waswahili… Mi ni mpwani AND AM NOT SWAHILI

SYCOPHANTS KUJENI MUONE!!! GOOGLE IMEITA AGWAMBO LORD RAILA

unfortunately at the coast like in many other places, watu watadanganywa kuwa Jubilee ndio imedhulumu watu wa pwani

:D:D:D:D