Hii ndio hekima ya ng'ombe pamoja na upumbavu wa kuku.

Hii ndo hekima ya NG’OMBE pamoja na upumbavu wa KUKU.

Ng’ombe, akishatoa maziwa ya kulisha familia nzima, hurejea katika malisho yake taratibu. Lakini kuku, akishataga yai moja hupiga kelele ili kila mtu ajue. Je! Yai hilo alilotaga laweza kutosha hata kwa mlo wa mtu mmoja? Jibu ni hapana.

Katika maisha kuna watu wa aina 2 kuna wale wanaofanana na Ng’ombe na wale wanaofanana na Kuku.

Mtu afananaye na kuku akikusaidia jambo hata kama ni dogo sana atasema kila mahali ili watu wote wajue jambo hilo. Kama ni kanisani/msikitini atahakikisha anajisifu sana na kuisambaza ile habari kwa wengi. Kuna watu walisaidiwa na watu hawa wenye tabia ya kuku baadaye wakaishia kuumizwa mioyo yao baada ya kusambaa kwa habari hiyo.

Mtu mwenye tabia ya kuku akitoa msaada hata kwenye kituo cha watoto yatima, au akisaidia maskini anatamani aje na waandishi wa habari.

Kuna watu wenye tabia ya ng’ombe. Akikusaidia hata kama ni jambo kubwa sana kiasi cha kushindwa kumlipa fadhila, hawezi kukusema na hataki watu wajue. Furaha yake ni kukuona unavuka salama na unafanikiwa. Watu wa namna hii hupata thawabu kubwa. Tamani kuwa na tabia kama hii ya kusaidia bila kujitafutia utukufu.

Hiyo tabia ya ng’ombe anayo BAKHRESA na tabia za kuku anazo Mzee Machache.

Niceeee…

Mungu atubariki tuwe na tabia kama ya Ng’ombe kwenye huu mfano wa uzi

Nimempenda Ng’ombe.

Aisee lakini Ni Kweli

ukipewa msaada na tabia kuku tafadhali ucupokee

We hujawahi patwa na shida wewe. Mtu akiamua kutangaza atangaze tu wala hainisumbui.

Kwa hiyo unataka kusema kuku anapenda sana publicity…

Wenyewe wakigundua…

Cc: @Mahondaw

Hahaaa

Kweli kabisa

Ng’ombe yuko vizuri

Kabisa mkuu

Aisee, ni kuuchunia sio

Kikubwa ushapata msaada sio?

Hahaa mkuu, mwanafasihi hafungwi

Naam, Rabeka!. Ila mwenzetu wewe umetumia mbinu gani hadi sasa cheo chako ni kikubwa begani village elder?

Kuku ni kuku tu