Watu wengi huwa wakizungumzia madikteta huwa wanazungumiza madikteta mamboleo, lakini dikteta wa kwanza (kwa mujibu wa Biblia) ni mtu anayeitwa Kaini, Kaini alitaka Mungu akubali sadaka yake na kuikataa sadaka ya Habili kwa kuwa tu yeye aliamini yuko sahihi kuliko Habili na Mungu.
Madikteta wote huwa na tabia hizo hizo za Kaini kuamini kwamba wao wako sahihi wakati wote na wenye mafanikio yasiyotokana na wao, ni lazima waondolewa kwenye jamii wanazoziongoza kwa njia yoyote ile. Dikteta hutaka kuweka sheria na kanuni anazozikubali na zinazoendana na udhaifu wake wa kibinadamu.
Lakini hakuna Dikteta aliyedumu milele!