Hakika tukipata uhuru huko kwetu Serikari Itatambua.

Wana jamii.

Unajua nimekimbia leo leo sasa kabla sijazoea maisha ya huku.

Nimegundua matabia mengi mabaya ya wenyeji wetu.

Matusi.

Mabifu

Uhuni.

Lakini kizuri ni Uhuru usio na mipaka.

Shime Nchi yangu ya Tanzania Mkiendelea na Udicteta wenu Tukirudi huko tutakuja na matabia ya Kimapinduzi na Kidemokrasia., wengi tutakuwa majasiri na wapambanaji kwa ajili ya uhuru wa Kujieleza tuliokuwa nao.

Wewe umeona nini?

NB: Wengi hawajatembelea kwenye majukwaa yao hawa Wa Kenya. Tembelea uone ujifunzi kitu.

Tupate uhuru wa kimtandao mara ngapi?, mpaka sasa tumeshapata tayari:
1: KenyaTalk (uhuru ni 100%, kwa sababu ya forum platform inayotumika ya XenForo, ni mojawapo ya platform zinazoaminika duniani kwa usalama)
2: BongoForums (ni forum ambayo siyo ya Tanzania, kwa hiyo TZ haina mamlaka nayo).

Mkuu hii bongoforums site yake ni ipi?

Site yake ni:
www.bongoforums.com

Nani aingie kwenye mtego wa panya wapambane na hali zao

Haahaaa mkuu mkimbizi2018 umenifanya nicheke kwa sauti usiku wa manane huku wife kalala:D:D:D

Unajuaje kama ni mtego?, ila serikali yetu dhaifu sana, maneno kidogo tu, wanareact kwa maamuzi ya kisirani. Uamuzi walioufanya kwa JF umeleta hasara kubwa kwa taifa, hasara yenyewe ni raia kutopata mbinu bobezi zilizopo JF, madini yote yaliyo JF sasa hayapatikani.

Hawataki kukosolewa

Serikali yangu ilipo kosea ni kuzuwia watu wakose pakutolea povu lao, mwisho wa siku watu tutajikuta tunatolea povu huku ugenini na madhara yake yatakua ni .akubwa zaidi kuliko tungetolea povu ama kuikosoa serikali kule nyumbani (Jf).
Wanasahau kwamba wanapo zuwia maji yasitembee mtoni, lazima majiyale yata jitafutia pa kupita.
Hapa ugenini tutajikuta hata majirani zetu wanaanza kujua udhaifu mkubwa unaofanywa na viongozi wa huko kwetu, na pia kuna wabobezi wa habari za uchunguzi kama akina Mohammed Ally, watapata mwanya mkubwa wa kuitangazia Dunia jinsi jiwe lilivyo gumu huko kwetu pamoja na kokoto zake.
Najiskia hasira tu aiseeeee…
Ebu niishie hapa kwa sasa

Ukimzuia mtu kwenda choo na haja kubwa imemkamata kisawasawa madhara yake anaweza achilia kimba :meffi::meffi: Hata sebuleni:D:D:D:D

Nisawa na kulazimisha mishuzi, mwisho wake ni kujinyea tu…tehteehhh

:D:D:D

Mbona site imekaa kisisemu sisiemu. BORA UKIMBIZINI TU

Site ina members 82

Hii site yaelekea ni mpya kabisa,itakuwa ipo kimkakati!

Watakula vichwa vya kutosha, ndio maana yenyewe haijafungiwa. WASIWASI NDIO AKILI

Ila site iliyojaa watu wenye mtazamo wa aina moja,mafisiem only, haiwezi noga mkuu.Ni sawasawa na TBC kila siku habari za magufuli na CCM yake,Siku wapinzani wakipewa airtime kuongea kwa Uhuru utaona nchi itakavyozizima kwa furaha!

Watanzania lazima tujihadhari na hizi blog mpya isijekuwa ni mtego…kwani hata usalama wa taifa wa Tanzania wanaweza kufungua vitu kama hvi

Mh!
Kwenye forum mpya kama hiyo ya BF comment kimachale.
Serikali imeshaua biashara ya online discussion forum, yeyote atakayefungua atakosa wateja, kwa sababu itaonekana siyo salama.

Uaminifu ni kitu bora sana kwenye biashara na mello amelionesha hilo