Habari Njema Kwa Wana JF, Ukimbizini Ugenini, JF Yetu ya Home, Bongo, TiiZii, Imerudi Hewani!, Japo...!.

Wanabodi wa JF huku ukimbizini, ugenini, ile JF yetu ya home, TiiZii, imerudi hewani!.

Japo hakuna kutufe cha kuposti new thread, hata kusoma tuu threads za zamani na kugonga like, sisi wengine, tunaridhika.

Pongezi JF Management Kuirudisha JF hewani.

Swali La Uzalendo Kwa Wana JF, Ukimbizini na Ugenini, Jee Tuanike Tuu Dirty Linen Zetu Kibarazani?, Au Uani Ili Kuhifadhi Aibu Yake, Aibu Yetu?.
Paskali

Mimi mtu ni bora uninyime maendeleo ya vitu lakini niwe huru, kunipa maendeleo ya vitu kisha ukaninyima uhuru wangu wa kufikiri na kutofautiana na wengine nitaendelea kukuona mjinga sana, hivyo ni bora kuanika mabaya ambayo ni ukweli ili watu wajue tuko na mtawala wa aina gani katika taifa hili

Tuanike tu hamna namna, wangejua hivyo wasingetufanya wakimbizi

Huyu magufuli hawezifanikiwa endapo ataminya Uhuru Wa kujieleza.wenzetu wazungu wameweza kuendelea kwa sababu ya ukweli na uwazi sasa magufuli amejaribu kuficha ukweli Wa bombardier lisu alipoanika nje magufuli akaamrisha auawe

Ngoja LEO niingie kuangalia thread za wakenya!!

Mkuu @Pascal Mayalla hizi dirty laundry zisipoanikwa zitatuozea huku ugenini. Inawezekana tukawa martyrs na kuwahi ile nafasi vya kuongoza malaika kabla ya the main applicant lakini tumesema ukweli.

Hata kama tukiendelea kukaa kimya huku kijijini mjini tukirudi wale wajumbe wa nyumba kumi hawawezi kuturuhusu kujiachia kiasi kile cha miaka ile kabla ya kuzimwa analogy na sasa wanajiandaa kutuletea Digital.

So naona ili tuendelee kusaidia watu kimawazo hatuna budi kualika wengine waje kijijini huku tujadili ya msingi na mjini basi tuendelee kufurahishana na chit chat tu lakini nondo za uwazi na ukweli zinapaswa kuwekwa huku kijijini.

Nina mashaka sana na mabalozi maana mwanzo tu walikuwa wanaedit heading za nyuzi zetu je wakati wa vigezo na masharit kuzingatiwa unaweza weka uzi na usiusome hata wewe mwenyewe.

Anguko la Jf kama wasipokuwa makini na mikakati yao basi ule utabaki kuwa mtandao wa watoto wanaobalehe kama ilivyo facebook hakuna la maana utalolikuta

Anyway tusubiri tuone maamuzi yao kuhusu sera zao mpya zitakuwaje

Mods wa huku wapole huu uzi wa 100 kuanzishwa kuhusu JF kurudi. Bora wale wa JF walikua wanaziunganisha kweli walikua na haki kufanya vile

Paskali kama kuna mazuri huko nyumbani hakuna anayekatazwa kuyaanika hapa. Ila sioni namna utazuia wale wanaotaka kuyataja hayo machafu. Mwenye mazuri akisifiwa ajidai apendavyo, na mwenye machafu akasafishe hayo machafu yake.

Jf is back,mbona hiyo ni throwback??..

Mazuri yakiwepo yasifiwe na mabaya yakiwepo yakandiwe
Nalog off

Pascal umesikiliza mahojiano na Maxenzo Mello jana saa mbili usiku Azam TV na Kamuntu (Mrs)…
One: Mello anasema ameshasajiliwa, kinachogoma ni mtu wa kusaini ambaye haonekani na this is tangu 15/06/2018.
Two: Wako kwenye mazungumzo na TCRA kuhusu kipengele cha tano cha maudhui ya mitandao kinachohusu to disclose source of information to police and any other “authorized authority”; … etc.
Three: Kamuntu alimbana akasema kama msipokubaliana na kipengele hicho ndiyo kusema JF basi? Jibu: No tutaenda hewani hivyo hivyo.
Hope: kama kungelikuwa na independent judiciary, kipengele hicho kinapingana na Katiba, hivyo ni rahisi kushinda mahakamani, lakini… we have a dead judicial system (ukiacha a few judges ambao wako determined kutunza haki/independency)

Hopefully wewe na Mello mnawasiliana, call him! amefafanua kuwa amefungua with limitation at least watu waweze kusoma past information before 10th June 2018 ambazo waliziweka @Pascal Mayalla

Wakiziacha kinaharibika nini? Ukikuta repeated information unaruka, unaacha… you proceed mbele

Umenena vema

U see na wewe sijaona umuhimu wa kuniquote mapovu ya nini wakati uzi sio wako ng’ombe hii kiherehere tu pheeeww

Paskali bunge la Kenya linakuita

Inakuwaje kila mtu anaanzisha uzi wenye mada ileile iliyoanzishwa na wengine zaidi ya kumi? Inamaana hawasomi wengine wameposti nini?..

Dah,
Wewe ndio umeiona saa hizi Mkuu??
Mbona kuna threads nyingi tayari zinazozungumzia kurudi hewani kwa JF?
Saa zingine heri uwe tu mchangiaji wa mada za members wengine kuliko kua muanzisha mada ambazo tayari wengine wameshazianzisha

Kuna watu hujiona wao ndio wanatakiwa waanzishe mada always kisha ndio zichangiwe na wengine