Ethiopia kuleta umeme wa bei nafuu, asema Rais Magufuli

[SIZE=6]Ethiopia kuleta umeme wa bei nafuu, asema Rais Magufuli[/SIZE]

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/3873162/highRes/1605416/-/maxw/600/-/13qqyph/-/ethiopia_Magu.jpg

http://i.imgur.com/TMIdW84.png

Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakiangalia vikundi vya ngoma baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Dar es Salaam jana, Picha na Anthony Siame

[SIZE=4]Kwa ufupi[/SIZE]
Ethiopia ilikubali kutoa kiasi hicho cha umeme kwa Tanzania katika mradi wake mkubwa wa umeme wa Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha MW 6400.

Advertisement
By Peter Elias na Kalunde Jamal, Mwananchi [email protected]
Dar es Salaam. Tanzania itapata umeme a megawatt 400 kutoka Ethiopia baada ya Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Hailemariam Desagen kukubaliana kushirikiana katika mambo 13.

Mbali na umeme, masuala mengine ni usafirishaji wa anga, bandari, matumizi ya Mto Nile, vibali vya kufanya kazi ndani ya nchi hizi mbili, utalii, kilimo, uboreshaji mfumo wa kodi, elimu, viwanda, madini na mazoezi ya riadha.

Ethiopia ilikubali kutoa kiasi hicho cha umeme kwa Tanzania katika mradi wake mkubwa wa umeme wa Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha MW 6400.

Makubaliano hayo yamefikiwa jana wakati wa mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mawaziri kutoka pande zote.

“Wamejenga dam (bwawa) linaloitwa Gibe Dam inayoweza kutoa megawatts 1,870. Na wanajenga sasa hiviu dam, moja kubwa kuliko dam yoyote katika Afrika inaitwa GERD inayoweza ku-produce megawatts zaidi ya 6,400 za umeme,” alisema Rais Magufuli.

“Ukitaka kujenga uchumi wa viwanda, lazima uwe na umeme. Wenzetu Ethiopia wametuonyesha njia. Na mimi nimemuomba.”

Alisema Desagen amekubali maombi hayo ya umeme huo ambao utakuwa wa bei nafuu na hivyo kulipa Shirika la Umeme (Tanesco) changamoto.

Mazungumzo hayo yaliambatana na utiaji saini wa mikataba mitatu ambayo ni wa mkakati wa ushirikiano kati ya Tanzania na Ethiopia ambao unalenga kupambana na tatizo la wahamiaji haramu, biashara na uwekezaji na ushirikiano katika sekta ya afya.

Mkataba mwingine ni kuanzisha kamisheni ya pamoja ya kudumu baina ya serikali ya Tanznia na Ethiopia ambayo itahusisha wizara za mambo ya nje za Tanzania na Ethiopia na kushirikisha sekta nyingine. Mikataba hiyo ilisainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Dk Workneh Gabeyehu na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Dk Suzan Kolimba.

Pia, serikali hizo mbili zilitiliana saini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya utalii ambao utatoa fursa ya za uwekezaji wa pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii. Mkataba huo ulisainiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia, Dk Hirut Teketel.

Rais Magufuli pia alizungumzia makubaliano baina ya mashirika ya ndege ya Ethiopian Airways na ATCL, akisema shirika hilo la Ethiopia sasa litageuza Tanzania kuwa kituo chake kikuu cha mizigo.

Alisema uamuzi huo utasaidia nchi zote mbili, ikiwa ni pamoja na Ethiopia kuanza kutumia Bandari ya dar es Salaam kupitishia mizigo yake kwa kuwa nchi hiyo haijapakana na bahari.

“Shirika la Ndege la Ethiopia ni kubwa sana, lina ndege 96 na wameagiza nyingine 42. Ndege zao zinatua katika viwanja zaidi ya 92 duniani kote. Hii ni nafasi kwetu kujifunza kutoka kwao ili tuongeze mapato yetu,” alisema.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Desalegn alisema Tanzania na Ethiopia zina uzoefu tofauti katika kukabiliana na changamoto, hivyo wana wajibu wa kubadilishana uzoefu huo ili kujiletea maendeleo.

Alisisitiza kwamba ni muhimu kuboresha kilimo kwa sababu wananchi wengi wanategemea kilimo. Alisema endapo serikali zitafanyia kazi suala hilo, zitakusanya mapato mengi kupitia wakulima hao.

“Asilimia 70 ya nguvu kazi katika nchi zetu ni vijana chini ya miaka 35, tukiwatumia hawa tutapiga hatua kubwa kwa sababu ndiyo nguvu kazi ya ujenzi wa Taifa lolote,” alisema Desalegn na kusisitiza kwamba Tanzania na Ethiopia zimekuwa na historia inayofanana.

Lugha ya Kiswahili

Kuhusu kuendeleza lugha ya Kiswahili Rais Magufuli alisema amejitolea kutoa maprofesa na walimu kwenda kufundisha lugha hiyo nchini Ethiopia.

Alisema amefikia uamuzi huo baada ya kukubaliana na Dessalegn kuwa akifika Ethiopia atachagua chuo kimoja cha kufundisha lugha hiyo.

“Kiswahili ni lugha ya Afrika, na kwa sababu makao makuu ya Umoja wa Afrika hayataondoka Ethiopia na yeye ni mtawala, pale Addis Ababa si vibaya akichagua chuo kimoja kwa ajili ya kukuza Kiswahili,” alisema.

Alisema miongoni mwa makubaliano yao pia ni katika kilimo, kwa sababu uchumi wa viwanda unaendana na kilimo endelevu kwa ajili ya kupata malighafi za viwandani.

Pia alisema Ethiopia pia itaisaidia Tanzania katika kupata njia za kunufaika na mashirika ya mawasiliano ya simu kutokana na mafanikio iliyoyapata kwao.

kwa tanzania, kila siku ni sikukuu ya wajinga, congaratulations are in order…

Kuna English version? Mimi nime elewa hiyo map pekee

Ulilipa karo kila mwaka na kusoma lugha ya taifa hukujifunza ? A shame !

3 Likes

hizo transmission lines zisipitie kenya

1 Like

Why do you think the power line will pass through zoomalia?

WaKenya wataiba umeme wao. [SIZE=1]Typical danganyikan mindset.[/SIZE]

5 Likes

Tanzania is the retarded cousin in the EA family.

3 Likes

http://eappool.org/wp-content/uploads/2016/01/EAPP_FrontLogo.jpg
EASTERN AFRICA POWER POOL (EAPP) IS A REGIONAL ORGANIZATION ADOPTED AS SPECIALIZED INSTITUTION OF COMESA FOR THE ELECTRIC POWER SECTOR.

The Eastern Africa Power Pool (EAPP) was established in 2005 with the signing of an Inter-Governmental Memorandum of Understanding (IGMOU) by seven Eastern Africa countries, namely: Burundi, Democratic Republic of Congo (DRC), Egypt, Ethiopia, Kenya, Rwanda and Sudan. In further development, EAPP was adopted as a specialized institution to foster power system interconnectivity by the heads of states of the Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA) region. Tanzania, Libya and Uganda have joined EAPP in March 2010, February 2011 and December 2012 respectively.

MANDATE
Our main objective is the optimum development of energy resources in the region and to ease the access to electricity power supply to all people of the countries in the Eastern Africa Region through the regional power interconnections.

EAPP GOALS

[INDENT][ul]
[li]To be a framework for pooling energy resources, promoting power exchanges between utilities in Eastern Africa and reduce power supply costs based on an integrated master plan and pre-established rules (Grid code).[/li][/ul]
[ul]
[li]Optimize the usage of energy resources available in the Region by working out regional investment schemes in Power Generation, Transmission and Distribution.[/li][/ul]
[ul]
[li]Reduce electricity cost in the Region by using power systems interconnection and increasing power exchanges between countries.[/li][/ul]
[ul]
[li]Provide efficient co-ordination between various initiatives taken in the fields of power production, transmission as well as exchanges in the Region.[/li][/ul][/INDENT]

1 Like

lakini kupitishia ZOOmalia si ni kupelekea alshaitan stima

from Somalia how will it connect to TZ?

si itaswim kwa indian ocean

1 Like

power buoys, undersea fiber…

Ile nyani ikiingia tena kwa sub station itazima stima ya inchi tatu, Ethio., Ke. na Tz. ama @inzhener otmetka kuja explainia sisi

6 Likes

are you suggesting mod fulani awekwe GPS monitor:)?

6 Likes

How many kilometers from the mainland because last time i checked, we have international waters.

1 Like

:D:D:D:D:D:Dkuwa serious kilometric, kwani una ka hangover?

Ndio naamka…

1 Like

Magafool kweli ni mjinga

Apigwe chain kwa shingo to restrict movement na supply ya bananas kwa wingi.

1 Like