Eid Mubaraq

Assalam alayqum wakimbizi wenzangu na wenyeji wetu humu

Eid Mubaraq alhamdulillah mfungo umeisha vyema, Allah atukubalie funga zetu

Amiin

minal faiidhina

Mwezi umeenda kama unasukumwa vile hatumae huoo majaaliwa mwakani inshallah Allah akijali

Mtukaribishe. Japo hatukuwasaidia kufunga.

Minal faidhina…

Subhi njema wadau

Subhi njema wadau, nawapa zangu salama
Nakupiga yangu mbiu, nawatangazia pema
Kundini bila dharau, na darasani twasoma
subhi njema wadau, nawapa zangu salama.

Siku hii Ijumaa, hatutaenda shuleni
Habari zimesambaa, tukwamie vituoni
Gauni lako kuvaa, jeupe tia chumbani
Subhi njema wadau, nawapa zangu salama.

Id twasherehekea, sote sote kwa pamoja
Msikitini fikia, namtaka kila kaja
Maulana twaombea, pirau kulia paja
Subhi njema wadau, nawapa zangu salama.

Oooh!

Shukrani mkuu

Eid el minal faidhina kwa wote.