Duale apigwa chenga na Kiswahili

Lugha ya Kiswahili imekuwa lugha ya kujivunia katika maongezi ya Mara kwa Mara lakini ueledi wa matumizi yake unazidi kuwakanganya wakubwa kwa wadogo, matajiri kwa maskini na hata wanasiasa.

[B]Leo katika kongamano la wajumbe wa chama kipya cha Jubilee pale Kasarani, Aden Duale amejaribu kutumia msemo mmoja wa Kiswahili wa kawaida lakini akakiboronga Kiswahili kabisa!!

Duale: ’ …meli ya Jubilee sasa imenanga!'( @introvert kuja na tinga).
Kwenye matumizi ya huu msemo, tunasema:

  • Kung’oa nanga(kuanza safari kwa meli hasa kutoka bandarini ama ilipokuwa imetia nanga).
    -Kutia nanga(kusimamishwa kwa Meli katika bandari au sehemu nyingine kwa minajili ya kupakiwa au kupakuliwa kwa shehena).

Nanga ni kifaa chenye uzito mwingi ambacho hutumiwa kusitisha meli ikiwa bandarini.Kifaa hiki huvutwa wakati meli inataka kuondoka bandarini na kuendelea na safari. Kwa kiiingereza kinajulikana kama ‘anchor’.

Kwa hivyo matumizi sahihi ni ‘Chama cha Jubilee kimeng’oa nanga!’…au labda kimetia nanga!'[/B]

7 Likes

Hata ndiye huyu Duale na masikio yake.
[ATTACH=full]56670[/ATTACH]

10 Likes

Meli=boat
Ship=
Yacht=
Canoe =
Aircraft carrier =
Submarine =
Saidia bro.

1 Like

Kiswahili pelekea wa TZ

1 Like

APAN TAMBUA KISWAHILI

1 Like

Hehehehe nilimskia, nikacheka.

2 Likes

Mashua = Boat

Ship = Meli

Yatch = Yoti

Canoe = Ngaramba/ matumbwi

Aircraft Carriers = Meli za kivita

Submarine = Nyambizi

5 Likes

Sante kwa mafunzo.

Hapa je

Shillingi 11,000
Shillingi 10,001

Kwa kiswahili sanifu

kwa sekunde kadhaa nilichanganyikiwa maana yake!!

1 Like

he can speak better English than you

1 Like

[B]Nilikuwa nimeandaa somo sawia na swali lako @Meria Mata lakiniMata lakini @Slartibartfast amejaribu kwa majibu yake.
Hata hivyo haya ndiyo majibu;

Ship=…Meli
Yacht= Yoti (utohozi was Moja kwa moja)
Canoe = ngalawa au kihori au mtumbwi au kipera.
Aircraft carrier = Mali za kubebea ndege za kivita.
Submarine = Nyambizi.
Boat…Nashua au ngalawa.
Dhow…Dau au jahazi.
Ark…Safina.
Steamship…Meli au merikebu.

Nataraji uko sawa.

[/B]

1 Like

Hatulijadilii hilo. Kwa kiingeraza ako na kongole zake kaka.

Shukran kaka, njoo sukari nikupe import, ningeeda mwiki lakini @imei2012 alihama

1 Like

Nitapitia unipe Pasi nyerezi ya huyo ‘import’ kaka.

Huo ni udhanifu wa kijumla kaka. Kiswahili cha watanzania wengi (kama wakenya) kimeadhiriwa na lugha zingine zinazosheheni katika mandhari ya makazi yao.

Kuna wimbo ya nyambizi tbt

Nitaurejelea huo uzi niusikize huo wimbo.