Dkt. Mwigulu Nchemba apendekezwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia, amelipendekeza jina la Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi huo unafanyika kufuatia taratibu za kikatiba ambapo jina la mgombea huwasilishwa kwa Bunge la Tanzania ili kupigiwa kura na wabunge.


Baada ya pendekezo hilo, wabunge watapiga kura ili kuthibitisha au kukataa uteuzi wa Mwigulu Nchemba kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwigulu Nchemba alizaliwa tarehe 7 Januari 1975 katika Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida. Alisoma elimu ya msingi na sekondari mkoani humo kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambako alipata Shahada ya Kwanza ya Uchumi. Baadaye alipata Shahada ya Uzamili na Uzamivu (PhD) katika fani ya uchumi katika chuo hicho hicho.

Kabla ya kuingia rasmi kwenye siasa, Mwigulu alifanya kazi kama mchumi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) .

Mwaka 2010 aliingia kwenye mbio za kugombea ubunge kwa mara ya kwanza na kuweza kushinda kwa kishindo kuanzia kura za maoni ndani ya chama hadi uchaguzi mkuu na kuwa mbunge wa Iramba Magharibi.

Amehudumu katika wizara kadhaa muhimu serikalini, zikiwemo:

  • Naibu Waziri wa Fedha (2012–2014)
  • Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika (2014–2015)
  • Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (2016–2018)
  • Waziri wa Katiba na SheriaMei 2020 hadi Machi 2021
  • Waziri wa Fedha na Mipango (kuanzia 2021 hadi sasa, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan).

poo GIF