ANSBERT NGURUMO AMEWAVUA NGUO
Mnasema mmefanya mazuri mengi ndani ya miaka mitatu? Ngoja niwaeleze kwa ufupi. Kitu pekee mlichofanikisha ni propaganda.
-
Mnanyamazisha wengine ili mseme peke yenu, lakini hamueleweki, wala hamkubaliki. Mmeona Twaweza walivyowaumbua!
-
Mnanunua ndege mbovu, tena kwa dili, mnasema ni mpya. Na mnazishangilia kama mazuzu; kumbe hata mpango wa biashara hamna.
Ndege inakorofisha ndani ya mwezi mmoja, mnasema inatengenezwa WiFi.
-
Mnasema hamna hela ya kurusha Bunge Lve, lakini mnapata za kurusha Magufuli Live.
-
Mnajenga kijibarabara cha zege, nacho chini ya kiwango, mnakiita flyover - taking advantage of Wananchi wasiojua flyover.
-
Bajeti yenu wenyewe mnashindwa kuitekeleza; Ikulu mnapeleka asilimia zaidi ya 400, huku kwenye Kilimo, Maji na kwa Wafugaji mnapeleka chini ya asilimia 10.
-
Mnaleta Makontena yamejaa Mali binafsi, mnaahidiwa kuyapitisha kinyemela, kwanza mnayakana; baaaye mnasema ni ya shule, lakini yameandikwa jina la mtu. Utapeli!
-
Mnashindwa kujenga Viwanda mlivyoahidi na mnabaki kusingizia kwamba vyerehani (4) vinne ni Kiwanda. Mnamdanganya nani ambaye mnadhani ni mjinga kiasi hicho.
-
Mnaua Raia na kuwatupa Baharini huku mkidai kwamba ni wahamiaji haramu - as if wahamiaji haramu wanapaswa kuuawa.
-
Mnaambiwa ukweli mnavua Watu uraia wao huku mkitishia kuyafunga Makanisa yenye Viongozi wa kiroho wasio wanafiki.
-
Mnazuia makinikia wakati Tanzanite na Dhahabu zinatoroshwa mchana kweupe, baadaye na hayo makinikia mliyoyazuia yanabebwa na wenyewe!
-
Hivi Noah zetu zimefika? Waongo wakubwa!
Yapo mengi. Kusema kweli, mmefanikiwa sana. Eti e?
Lakini mtambue kuwa kila mnapojibidisha kuudanganya umma, wa kwanza mnaowadanganya ni nyie wenyewe mnajidanganya.
-
Mnaondoa wasio na vyeti, mnawachomeka ndugu zenu walioiba vyeti vya wengine, tena wasiojua hata kusoma “A.”
-
Mnashindwa kufariji waliopigwa na tetemeko na kupoteza ndugu zao, baadaye mnawapora wahanga hata rambirambi wanazosaidiwa na wenye huruma. Laana inawatafuna!
Nasema hivi, mimi Ansbert Ngurumo nayasimamia haya sasa na miaka mitano ijayo na zaidi ijayo. Kadiri muda unavyosogea, ndivyo ukweli unavyozidi kuanikwa, na nyie mnazido kuumbuka.
Mtafika mahali mtapigwa na propaganda zenu wenyewe.
Huyo jamaa akishaondoka madarakani, watakaokuwa wa kwanza kumshambulia ni nyie mnaomlambalamba leo. Unafiki!