Dictator hujenga vidictator vyenzake katika mfumo ili afanikiwe

Nimesikiliza press conference ya Chadema, Mh. Freeman Mbowe akiongea kuhusu ‘vituko’ wanavyoshuhudia mahakamani. Moja kati ya mbinu za madikteta wa Afrika ni kutumia vyombo vya dola na vile vya kisheria katika kudhibiti wapinzani wao wa kisiasa. Aghalabu wasaidizi wa madikteta hupatikana katika vyombo hivyo, wanaweza kuwa wakuu wa vyombo vya dola, majaji na mahakimu, na wateule katika nafasi za uongozi wa kiserikali.

Adolf Hitler aliwaua binadamu milioni 6, karibu nusu ya hao walikuwa wayahudi. Alifanikiwa kupandikiza chuki dhidi ya wayahudi na kwa hiyo ilirahisisha mauaji. Unadhani, Hitler aliwaua watu wote hao kwa mkono wake? Haiwezekani. Aliagiza wanaomuunga mkono, na hao wanaomuunga mkono walitekeleza mauaji dhidi ya watu wanaowachukia, hata bila Hitler kujua.

“Dikteta husambaza chuki yake kwa kuambukiza vidikteta vyenzake ndani ya Jeshi, Polisi, Mahakama, jamii nk”.

Tulifundishwa shuleni, kwamba kuna mihimili mitatu ya nchi, ambayo ni Serikali Bunge na Mahakama. Panapotokea Dikteta dhana hiyo inakufa. Badala yake tunakuwa na Serikali, Serikali na Serikali.

Dikteta haamini katika Ugatuzi wa madaraka, yeye kichwa chake ndio katiba ya nchi, na ukifanya tofauti na apendavyo unakiona cha mtema kuni. Kwa hiyo ili uendane naye, unatakiwa kuwa “Coward” kwa maana ya kutenda tofauti na fikra zako kwa sababu ya woga, au labda na wewe uwe kidikteta kidogo kwa maana ya kuwasilisha na itikadi kama za huyo dikteta kubwa.

Huyo hakimu Mashauri anayetajwa kutumiwa kutaka kuwafunga akina Mbowe, anaangukia katika moja ya makundi hayo mawili.

Kitu gani kitatokea ikiwa wananchi wataona kwamba mahakimu na majaji ni “wasanii”, na kwamba wanafanya kazi kwa kufuata itikadi zao, au kuelekezwa? Mahakama itapoteza mvuto na imani kwa wananchi. Kwa hiyo, vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vitaongezeka, hasa kwa watu wa upande unaoonewa. "Kwanini nikupeleke mahakamani wakati wewe ni mwanachama wa chama pendwa na mimi ni mtengwa, na hakimu anaelekezwa na m/kiti wa chama chako badala ya utashi wa kitaaluma?

Askari wanaua watu halafu wanabambikizia kesi watu wengine kwa maelekezo ya mtu, na mahakama bila aibu inafuata…Kuna haja ya kuwa na mahakama katika mazingira haya?

Tumalizane huku huku mtaani. Who cares?

Mtazamo wangu ni uleule, madikteta wengi ni watu dhaifu na waoga. Bila madaraka, mtu mwenye akili za kidikteta anatia huruma sana. Ndio watu wa kujipendekeza, na wakishapata nafasi, utawakoma. Mifano ipo tele.
Lakini kuwa na akili za kibabe katika dunia ya leo, ni ishara ya ujinga, ushamba, upumbavu na ulimbukeni wa kiwango cha juu kabisa.

mr mkiki .

Tatizo kubwa zaidi ni kuwa hakuna mwenye akili timamu atakaewekeza nchi hii tena (si wakati huu wa jiwe bali hata siku nyingi zijazo). Wafanyabishara wakubwa na wadogo huingia mkataba wakijua wanafanya biashara na mtu wasiekuwa na uhakika nae kama ni mwaminifu. Lakini kukiwa na mahakama zinazoaminika watapata ujasiri wa kujaribu kufanya biashara wakijua kuwa likitokea la kutokea wataipata haki yao mahakamani. Hali inakuwa nzuri zaidi pale ambapo serikali inaheshimu maamuzi ya mahakama (kwa kutoingilia process nzima na kuheshimu maamuzi yaliyotolewa leo na keshokutwa).

Magufuli anaiua nchi hii huku watu wakishangilia

Mawaziri wote, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, polisi, DEDs, etc wote ni vidictaitor vidogo ambavyo vinafanikisha Udikiteita wa Dictaita mkubwa.

Hivi hivyo vidikteta vina ulinzi kila mahali? Ni wazo tu limenijia.

Idd Amin angeishambulia nchi hii leo jumatatu (with the same quality ya jeshi alilokuwa nalo Uganda in 1978 but with ours as it is today) by Sunday of the same week angekuwa Dodoma.
Nadhani nimejibu wazo lako

Nimekusoma mkuu tena kwa herufi kubwa. Ngoja wazidi kumuendekeza jiwe wakati ukifika hawatamuona.

Inasikitisha sana…

Kuna mambo yanaonekana rahisi rahisi ila impact yake ni kubwa sana…

Cc: @Mahondaw