Nawasalimu wote kwa hisani ya majirani zetu Wakenya wenye uhuru wa kweli. Na kweli humweka mtu huru.
Kila mtu anajua kuwa kwa mila za Kiafrika hasa Tanzania ni jambo la aibu na fedheha baba mzazi kumwingilia binti yake wa kumzaa.
Katika dhambi isiyovumilika ni hiyo na huweza kupelekea hata binti aliyeingiliwa kujiua kukwepa fedheha atayoipata kwa jamii.
Tanzania ya leo imeanza kulaaniwa kwa matendo yasiyofaa kama haya ya kuwaingilia mabinti wa kuzaa wenyewe aidha kwa kuwalazimisha au kwa kuwarubuni vyote havikubaliki. Matukio haya yamekua yakitokea sana ktk jamii zetu na yamekua yakifumbiwa macho kwa kuhofia kubambikwa kesi na wahusika hasa wakiwa ni wakubwa kwa maana wenye vyeo vitukufu.
Nimalizie maoni yangu kwa kuwaasa wote waliofanya mchezo huu watubu haraka sana ili nchi yetu ianze kukua kiuchumi, kijamii, kisayansi na kitekinolojia.
Pia nawakemea wote wafanyao mchezo huo wakome mara moja, hii ni fedheha jamani hata Mungu hapendi uchafu huu.
Mbarikiwe sana kwa hisani ya majirani zetu. Ndimi mkimbizi mwenzenu.
:oops::oops: nanukuu “Matukio haya yamekua yakitokea sana ktk jamii zetu na zimekua zikifumbiwa macho kwa kuhofia kubambikwa kesi na wahusika hasa wakiwa ni wakubwa kwa maana wenye vyeo vitukufu”:rolleyes::rolleyes:
Kama wapo wababa wa namna hii inabidi wanaume tuwatafute tuwasute. Heshima ya binti yangu inafanana sana na heshima ninayompa mama yangu mzazi. Ni karaha na inaleta ukakasi kusikia mambo haya ya kimapepo