Deorro njoo kidogo nikupe wosia!

Bwana mdogo babu yako @Art amerudi tena ila sikuwa nimeenda popote,nilikuwa mumu humu kijijini.Nimesha kwambia huwezi ukadhibiti mambo ya mitandao na kile kinachoendelea mule ndani,ikiwa magwiji wenye uwezo,stanashati na utenda kazi wa hali ya juu kama vile google hawawezi itakuwa mbilikimo kama wewe?
Bwana mdogo wacha pupa ya maisha ikiwa umetunukiwa mamlaka madogo kama ya kudhibiti nidhamu na maadili bora katika hiki kijiji yatumie hayo madaraka kwa uadilifu,staha na hekima.Tushaona wengi waliokuwa na mapepe kukuliko wewe lakini waliishia kupanda upepo wakavuna tufani.
Bwana mdogo natamatisha waraka huu kwa kukuonya ya kwamba usipokuwa mwangalifu,mpole wa mambo basi utaambulia patupu na aliyepakwa kinyezi usoni na majivu kwenye matako!lauhaula mimi sikuhukumu kamwe ila naelewa unakotoka na unakotokomea kwani wahenga walinena maskini kisha pata matako hulia mbwata!Yako yashalia kilichosalia ni kupasuka msamba.

37 Likes

Karibu @Art

General welcome back!

Sande Sana kwa mawaidha

Asante Ndugu zanguni!

Asante Kaka nimefurahi kukuona upo na uanendelea vizuri.

2 Likes

hii kiswahili ni mufti.

Wah! Swahili sio ya kila mtu. Karibu @Art

4 Likes

Asante dada,nafurahi kukuona tena.

[SIZE=5]Kwa walio lemewa na hio lugha[/SIZE]
[ATTACH=full]100123[/ATTACH]

27 Likes

…ati umesema akujie kidoggie? :eek:

:):)Auto translation mbovu sana

7 Likes

welcome back…your contributions are needed

Hali ilikuaje mle toharani? Karibu sana lakini.

Sikuwa nimeenda popote mie,nilikuwa mumu humu nikitumia kibubusa badala.

4 Likes

:D:D:D:D:D:D

This is akin to tickling the anus of a leopard.

9 Likes

ahahahahah,oh my gos!

Safi sana kaka, nasaha imeeleweka vizuri.

oh my sijawahi cheka hivo ati buttocks cry mbwata
[ATTACH=full]100131[/ATTACH]

3 Likes