DAWA YA UDIKTETA NI MAARIFA

Kama wewe ni kiongozi bora kwanini unaogopa kukosolewa kuna siri gani unayoficha ni kwa faida ya nani?

Kutumia vyombo vya dola na taasisi kubana wakosoaji ni roho mbaya ya kuzaliwa na sio kujifunza.

Kukataa kukosolewa ni dhana ya kukataa uwajibikaji na kulea udhaifu wa marafiki ambao umewatunukia vyeo pasi kuwa uwezo wowote wa kiutendaji.

Roho mbaya ya kuzaliwa ndiyo inakuongoza kuwanyima watu stahiki zao, kama kulipa mafao ya wastaafu, madeni ya ndani na kuchukua kapu la fedha kuzunguka nalo na kufanya show game ya kusaidia mtu mmojammoja ili kutafuta umaarufu.

Na kujifikiria kuwa wewe ni smart zaidi ya masmart wengine, huko ni kujilisha upepo na nia yako ya kurudisha muda nyuma mpaka zama za mawe hazitanikiwa.

jiwe lina roho mbaya kwelikweli,the first Tanzanian dictator. HOVYOOOO kabisa

Niwaangalia na kusema hiiiiiiii dawa yenu inachemka, mimi ni jiwe.

@The Tweet ihamishie jukwaa la siasa JamiiForums

Nani huyo’ ebu mtaje bob’ anasababisha watu mnakunywa chai kwa mluzi

Ashakuwa jiwe nyie mmebakia kuwa nazi tu

Kuna mawe ya chokaa huweza kuvunjwa na nazi

Hili bandiko lipelekwe tu jukwaa la siasa, huku wenyeji watapata shida sana kung’amua nini kimezungumzwa kwa kuwa kiswahili kilichotumika ni kigumu kwa wenyeji walio wengi.

Ndugu muwe na subira. Magu siku yake inawadia aondoke mamlakani. Hapa hapa Kenya tulimchoka kwa kuwa amejaribu kuvunja uhusiano mwema baina ya nchi jirani hapa Afrika Mashariki

Hiyo siku ikiwadia nitapika pilau ninywe na soda baridi.

@Sky Eclat, na usikose kunialika. TZ itavutia mkiwa huru

Jirani nitakualika na nitapika maandazi ya nyama kwa wingi sana.

Vumilieni kwa muda

Msemakweli mpenzi wa Mungu

Hata MUNGU na uwezo wake wote lakini hautumii vibaya kama hilo jiwe, kwani angeweza kumfuta shetani ili akae kwa amani lakini kakubali changamoto za shetani ili asilale usingizi, sasa yeye ni nani hata asikosolewe?

Atatokea tu mtu wa kutukomboa kama vile Daudi alivyompiga Goliath kwa kutumia nguvu za Mungu

Time will tell…

Cc: @Mahondaw

that animal is a giant of a fool

I shall throw a big party on that day

Dawa ya moto ni moto