Dar es Salaam. Mambo yamekuwa mambo mitandaoni. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kuvutana katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusu mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri.
Katika mabadiliko hayo yaliyofanywa na Rais John Magufuli, Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ameachwa.
Zitto aliandika katika ukurasa wake, “ndugu yangu Mwigulu Nchemba karibu back bencha ufanye kazi ya wananchi. Tunajua msimamo wako kuhusu barua ya KKKT (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania) umekuponza, ulikuwa na msimamo madhubuti na ulisimamia haki.”
Baada ya Zitto kuandika hayo, Polepole aliibuka na kumjibu, “mzee wa kurukia treni kwa mbele ushaanza, mbona unapenda ubashiri na vitendo vya kilozi. Rais hutenda impendezavyo kwa dhamana aliyopewa na Katiba.”
“Sisi tuliohudumu kwenye serikali na chama tunajua na kuheshimu, usijitatafutie huruma kwa mtu acha kupotosha hiyo si siasa safi.”
Katika mabadiliko hayo, nafasi ya Mwigulu imechukuliwa na Kangi Lugola ambaye awali alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
Tunapo elekea, hata hao anao wateuwa wataanza kugoma na kuzikataa nafasi hizi za kuteuliwa kwasababu hawana Imani na anae wateuwa, na anawafukuza kama mbwa… tehteehhh
Dhamana aliyopewa na katiba IPI? After all, “Katiba sio kipaumbele changu”… rejea maneno ya mkuu. Chakubanga huna hoja kabisa, sio lazima uandike kama huna cha kuandika!!
Chakubanga is really clueless and rudderless. Zitto amebainisha tu hisia zake. Chakubanga anarukia kumkataza kuwa hisia na kumkejeli! Hao ndio viongozi wetu! Ridiculous. No wonder Kinana ameamua kujiondokea.
Mkuu tukifikia huko itakuwa bomba sana. Unadhani huyu Mwigulu anaweza kuamua kupambana na dikteta chini kwa chini akishirikiana na MACCM wengine ili wampige chini 2020? Au atahofia?
Ni kizee fulani hivi kiropokaji hapo lumumba, ndiyo kilikuwa kidalali cha kununua wapinzani uchwara, kilipiga hela nyingi sana kwenye hiyo project kimestukiwa ndiyo maana manunuzi yamekoma.