CC: Mabenda. PASTA ADAI ASHAZUIA MVUA HATARI YA EL NINO

PASTA mmoja kutoka eneo la Ukunda kaunti ya Kwale amewaondolea Wakenya hofu dhidi ya uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa ya El Nino kuanzia Oktoba.

Geoffrey Mwariga ambaye pia ni mmiliki wa kituo cha mayatima cha Born Again Children eneo hilo anadai kuisitisha mvua hiyo kupitia maombi aliyofanya mnao Septemba 13, 2015.

Akiongea na waandishi wa habari nyumbani kwake, Bw Mwariga alisema kuwa mwenyezi Mungu alimpatia uwezo huo ili kurudisha imani wa waumini kwa viongozi wa kidini.

Aidha alidokeza kuwa alichukua hatua ya kusitisha mvua hiyo kwa heshima ya Mungu kwa sababu aliona ya kwamba serikali haina uwezo wa kuzuia uharibifu wake.

“Ningependa kuwaondolea wakenya hofu na serikali kwa ujumla ya kuwa hakutokuwa na El-nino kama vile ilivyotangazwa na idara ya utabiri wa hali ya hewa,” akasema Bw Mwariga.

Bw Mwariga alieleza kuwa iwapo mvua hiyo ingelinyesha basi ingelileta maafa makubwa zaidi ya wale ambao wamefariki katika ajali za barabarani, mikasa ya moto na kadhalika.

Aliongeza kuwa sababu kuu ambayo ilipelekea kukubaliwa kwa maombi yake ni msimamo wa Rais Uhuru Kenyatta dhidi ya kupinga ushoga na usagaji humu nchini.

“Wakati ambapo kiongozi wa nchi aliposimama na kupinga ushoga hapo ndio El-nino ilipotea kwa sababu ilibainika kuwa haungi mkono mambo ya kishetani,” akasema pasta huyo.

Pasta huyo alisema kuwa mvua hiyo haipaswi kuchukuliwa kama jambo la kawaida kwa sababu inatokana na roho ya uharibifu ambayo lengo lake kuu ni kusababisha uangamifu.

Nguvu za maombi

Alikariri kuwa kama vile viongozi wa kidini walivyofanikiwa kuzuia maafa yaliyokuwa yakishuhudiwa kila mwezi, kupitia maombi mvua hiyo pia imezuiliwa.

“El-nino inapokuja huwa kuna laana fulani ambayo imesababisha na njia moja ya kuondoa laani hiyo ni kujielekeza mbele ya Mungu na kutubia dhambi zetu,” akasema Bw Mwariga.

Wakati huo huo Bw Mwariga aliwahisi viongozi wengine wa kidini ambao wametwikwa jukumu la kuombea nchi wachukulie tahadhari zote zinazotolewa kwa uzito zaidi.

Alisema kuwa iwapo tukio lolote baya linaweza kujitokeza na kuleta maafa humu nchini ni ishara tosha wale ambao wamepatiwa mamlaka hawawajibikii majukumu yao.

“Bibilia inasema tukiwa na imani ndogo kama chembe cha haradai tutauambia ulima ng’oka tupwa baharini kwa hivyo sihitaji imani kubwa kusimamisha El-nino,” akasema Bw Mwariga.

1 Like

:D:D:D:D:D:D:D

Hii ni nyef nyef ya kuandaa shamba kwa wapandaji wa mbegu

2 Likes

i wonder where he will hide when el nino gets here

Hehehe. Sasa huyu si aombee dola ishuke dhidi ya shilingi. Aki "men of god " wana mambo.

4 Likes

Noah arc and the fools !!!

please aoombee walimu warudi chule

2 Likes

Does this guy understand what El Nino is? Is he even aware that its destructiveness depends on a scale, just like earthquakes, hurricanes etc.
Angesema ameombea makali ya El Nino yapungue.

1 Like

Hio Kiswahili…utanisamehe.

2 Likes

:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D:D
in my school kiswahili was optional but mother tongue was mandatory

2 Likes

hehe…hata mimi

1 Like

Kwa wale wako na tatizo ya kusoma Kiswahili:

PASTA one from Ukunda area of Kwale County has removed Kenyans fear against possible exposure to rainfall of El Nino in October.
Geoffrey Nariga who is also the owner of the orphanage Children Born Again of the area claimed that the rain stop it through prayer he did ye September 13, 2015.
Speaking to journalists at his home, Mr. Nariga said that Almighty God gave him the ability to restore the faith of believers in religious leaders.
In addition he noted that he took steps to terminate the rain to honor God because he saw that the government is not able to prevent its destruction.
“I’d like to relieve Kenyans fear the government as a whole that there will be no El-nino as announced by the department forecast the weather,” said Mr Nariga.
Mr Nariga explained that if the rain would bring major disaster ingelinyesha then most of those who have died in traffic accidents, fire disasters and so on.
He added that the main reason which led to the acceptance of its application is the position of President Uhuru Kenyatta protest against homosexuality and lesbianism in the country.
“At a time when the country’s leader and anti-gay stand at the El-nino was lost because it was found that does not support what the devil,” said the pasta.
Pastor said that the rain should not be considered as a phenomenon because it stems from the spirit of destruction that its main objective is causing destruction.
The power of prayer
Alikariri be as much as religious leaders succeeded to prevent the disaster that had witnessed every month, through the wet application also inhibited.
“El-nino comes there is a curse that has caused one way to remove it is to focus condemned before God and repent of our sins,” said Mr Nariga.
Meanwhile Mr Nariga he feel other religious leaders who took away the responsibility of praying for the country to keep away from all the attention provided more weight.
He said that if any unpleasant incident could happen and tragedies in the country, is a sign to those who have given the authorities do not wajibikii their duties.
“The Bible says we have faith as small as a grain of the Paradai will say to the mountains be moved thrown into the sea with great confidence that I need to stop El-nino,” said Mr Nariga
.

(from Google Translate)

7 Likes

Angeomba hiyo mvua inyeshe turkana

1 Like

hata mimi.

…ama ukambani

1 Like

Funniest crap i ever read. Nacheka ka fala ndani ya bank. Hehe

Mwariga becomes Nariga.
:D:D:D

Hata gugu inataka osungu.jpg

1 Like

Prof awour was there too akisema dunia inaisha blah blah

ndio hii ishafika siera leone, west africa

[ATTACH=full]15490[/ATTACH]

[ATTACH=full]15491[/ATTACH]

[ATTACH=full]15492[/ATTACH]

[ATTACH=full]15493[/ATTACH]

Noma sana.