Leo ndio leo hatimaye imefika siku muhimu kwa wapenda soka barani Africa
Ni fainali ya mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Africa kwa msimu wa 2022/2023 kati ya Yanga na USM Alger
Mechi hii itachezwa mnamo saa 10 jioni kwa saa za Africa mashariki kwenye dimba la Benjamin Mkapa.
Timu hizi katika historia zimeingia fainali kwa mara ya kwanza, na pia ziliwahi kukutana kwenye msimu wa 2018 ambapo Yanga alifungwa kwa hiyo mechi hii inaweza kuwa ya kisasi