Breaking News : Hiace Yagongana Na Lori La Mchanga Na Kuua Watu 14 Mkuranga

[SIZE=5]Breaking News : Hiace Yagongana Na Lori La Mchanga Na Kuua Watu 14 Mkuranga[/SIZE]

https://4.bp.blogspot.com/-qV7htqLu7B4/WzC76auQpaI/AAAAAAAB9eA/w5m8NEwto0QCx837H3lKsJAi8j5vz9ZbQCLcBGAs/s1600/1.jpg
Watu 14 wamefariki dunia na wanne kujeruhiwa baada ya daladala walilokuwa wakisafiria kugongana na lori.

Ajali hiyo imetokea leo Juni 25 saa 10 alfajiri katika eneo la Dundani wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Dk Stephen Mwandambo amethibitisha vifo hivyo, amesema maiti za watu 14 zimepokelewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo.

“Ni kweli hili tukio limetokea alfajiri, tumepokea miili 14 na majeruhi wanne,” amesema Dk Mwandambo.

Kati ya majeruhi hao, amesema mmoja hali yake ni mbaya na walikuwa wanahangaika kuokoa maisha yake.
https://3.bp.blogspot.com/-uZnMJmbkQHM/WzCo08w2VOI/AAAAAAAB9cw/bIG_dsNcB88BVNzhIsIlQ4Geik_WBYy_wCEwYBhgL/s1600/2.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-nlApYoi4cwY/WzCo06kEooI/AAAAAAAB9c0/Jyj784lRuF8mb6VrWzT6ofhUaO6Jvw2JACEwYBhgL/s1600/3.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-rVk7i4kyXdI/WzCo192gSfI/AAAAAAAB9c4/wa4nhZQcvjc468HKAULE-68vJjEFrsR6ACEwYBhgL/s1600/4.jpg

Kwa barabara hii ya kilwa hususani kuanzia kongowe serikali lazima ichukue hatua hasa kwa haya malori ya michanga kwani daaaa!!!wanaendesha kama ndio watumiaji pekee wa barabara!!hususani usiku kwani wengi wao wanakesha na ndio maana hata huyo aliyesababisha ajari alikuwa amesinzia!!!na wengi wanaoyandesha wanakuwa ni makondakta tu na sio dreva!!!yeye anataka umpishe hata akiwa anakuja upande wako wewe ndio uingie polini kumkwepa!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko taarifa ya vifo vya watu 14 waliopoteza maisha baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la kubebea mchanga katika eneo la Dundani Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Ajali hii imetokea tarehe 25 Juni, 2018 saa 10:40 Alfajiri wakati basi dogo lililowabeba wanafamilia, ndugu na jamaa waliokuwa wakielekea Msata kuhudhuria sherehe za kumaliza mafunzo ya kijeshi kwa mtoto wao, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Dundani kuchukua mchanga.
“Naomba unifikishie pole nyingi kwa wanafamilia wote waliopatwa na msiba, waambie naungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majozi ya kuondokewa na wapendwa wao, na sote tuwaombee Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi” amesema Mhe. Rais Magufuli katika salamu zake za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
Mhe. Rais Magufuli pia amewaombea majeruhi 4 wa ajali hiyo wapone haraka ili waweze kuungana na familia zao na kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
25 Juni, 2018

Kwa maana hiyo wamekufa abiria wote, ajali mbaya sana hii…pole kwa wafiwa.

God is great.

Mtukufu rais wa wanyonge ametoa salamu

R.I.P

Mhh! Had I jiwe limeguswa!

Mhh! Hadi jiwe limeguswa!

So sad…Tunakuomba Mungu Mwenyezi awape pumziko jema na majeruhi wote tunakuomba Mungu uwasaidie wapone

Kama Dereva wa Lori usiku mzima badala ya Kulala ili mwili upumzike vizuri Yeye anakuwa juu ya Kiuno cha ’ Malaya ’ huku akikatiwa Viuno vya kila aina unategemea ’ akidamka ’ asubuhi kuanza majukumu yake hatosinzia na kupelekea kusababisha hizo ajali?

Mkuu Eli kwanza natoa pole kwa wote waliopoteza ndugu zao na pole nyingi kwa Majeruhi. Na Mungu awapumzishe panapostahili marehemu wote. Hila mkuu tafadhari taharifa za huyo chogolee jiwe tunaomba huku zisiandikwe kabisa maana jamaa hana imani na mitandao na ndo kasababisha tupo ukimbizini kwa sasa. Huku habari zije lakini sio kuhusu huyo bwege bana.

Mhh

pamoja mkuu

anajifunza taratibu, sio siri aliukwaa bila kutegemea

Pole kwa wafiwa; hiyo bara bara magari huwa yanakimbia sana toka hapo vikindu kwenda Mkuranga.

R I.P

Pumzikeni kwa Amani ndugu zetu.

Jinafki tu, wala halijaguswa.

wapumzike kwa amani

Yaani wanafungia mtandao wetu halafu bado mnaleta taarifa zao huku. Hizi mngewaachia Uhuru, Jamvi la habari, Tanzanite, Daily news na Tazama bila kusahau tbc