BAWASIRI/MGOLO
Bawasiri ni ugonjwa unaotokea katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje.
Kwa kiingereza hujuliakana kama piles.
Na kitaalam hujulikana kama hemorrhoids
AINA ZA BAWASIRI
1⃣ BAWASIRI YA NJE
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina hii ya bawasiri kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
2⃣BAWASIRI YA NDANI
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu.
Aina hii imeainishwa katika mainisho ya madaraja manne yafuatayo:
Daraja la 1 - Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja la 2 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya haja.
Daraja la 3 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya haja.
Daraja la 4 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya haja.
www.sangidaherbal.blogspot.com
BAWASIRI HUSABABISHWA NA NINI?
Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa
Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu
Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.
Kuharisha sana kwa muda mrefu
Kutumia vyoo vya kukaa
Kunyanyua vyuma vizito
Mfadhaiko/stress
Uzito na unene kupita kiasi.
DALILI ZA BAWASIRI
Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote
ATHARI ZA BAWASIRI
Upungufu wa damu mwilini
Kutokwa na kinyesi bila kijitambua
Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
Kupungukia nguvu za kiume (kwa wanaume)
Kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
Kupata tatizo la kisaikolojia
NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI
Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi
Kunywa maji mengi lita sita hadi kumi na mbili kwa siku
Acha kufanya ngono kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.
Kwa ushauri na dawa za magonjwa mbalimbali wasiliana nami
www.sangidaherbal.blogspot.com
+255 655 821 550
Sulayman Sangida