Ash Wednesday tomorrow

NDUGU MKRISTO, KESHO SIYO SIKU YA KAWAIDA!

Sijui upo wapi sasa hivi, sijui umejiandaa vipi… lakini nataka nikuweke tayari kwa siku ya kesho! Kesho ni Jumatano ya Majivu – mwanzo wa Kwaresma!

Hii siyo siku ya kawaida, ni siku ya toba, unyenyekevu, na mwanzo wa safari takatifu ya siku 40 kuelekea Pasaka. Utakapopakwa majivu kesho, usione ni jambo la kawaida tu. Majivu hayo yanakukumbusha kwamba “Wewe u mavumbi na mavumbini utarudi” (Mwa 3:19). Yanakualika utubu, ujinyenyekeze mbele za Mungu, na kubadili mwenendo wako.

Ndugu yangu, Kwaresma siyo tu muda wa kuacha kula nyama au kufanya mazoea fulani. Ni kipindi cha kufungua moyo wako kwa Mungu, kujitenga na dhambi, na kujitoa zaidi katika maombi, kufunga, na matendo ya huruma.

Je, umejiandaa vipi?

Moyo wako uko tayari kutubu na kurudi kwa Mungu?

Umejipanga vipi kuifanya Kwaresma hii kuwa tofauti na zilizopita?

Una mpango gani wa kukua kiroho katika siku hizi 40?

Kesho tunapoanza safari hii, tusifanye ibada kwa mazoea. Tufanye kwa uaminifu, kwa bidii, na kwa toba ya kweli. Tuanze upya na Mungu!

Bwana akubariki na akuongoze katika Kwaresma hii. Tuanze safari ya utakatifu kwa moyo wa unyenyekevu!