Habari ndugu!
Natambulisha kwenu AI bot ya Telegram ambayo inaweza kushiriki kwenye mijadala mbalimbali ya groups za Telegram:
Faida za bot hii:
Kwa wanafunzi/wanachuo ambao wana_group za discussion kwenye Telegram watapata fursa ya kupata mchango wa moja kwa moja kutoka kwa bot pale ambapo watamtag kwenye hiyo conversation, lakinip pia wanaweza omba awape reference zaidi, afanye majuisho ya discussion au atoe maoni yake ktk mada inayo endelea.
Lakini pia, endapo umechelewa kuingia kwenye group, na pindi unapoingia unakuta SMS 50 au 100+ huwa inakuwa ngumu sana kusoma moja moja, hivyo unaweza mtag bot huyu na kumwambia akupe summary ya conversation iliyokuwa inaendelea, kisha ndani ya sekunde 10, bot atakupa summary ya conversation
Ili kumtumia bot huyu wa Telegram fuata hatua hizi
- Kama ni kwa matumizi ya group search @WaGPTBot kisha mu_add kwa group, baada ya hapo ukitaka bot achangie utaanza kwa kumtag mfano @WaGPTBot naomba nipe summary ya hiki kilicho jadiliwa hapa Kisha bot atafanyia kazi ulichomwambia
- kama ni kwa matumizi binafsi search @WaGPTBot au fuata link hii https://t.me/WaGPTBot kisha chat naye inbox moja kwa moja.
Next feature:
Tunafanyia kazi uwezo wa bot kutambua magonjwa ya mazao pale unapomtumia picha ya mmea mwenye magonjwa.
Ahsanteni sana.