Aina ya Wafadhili kwa Miradi ya Maendeleo (Categories of Donors for Development Projects)

https://www.awwa.org/portals/0/files/education/conferences/seminars/graphics/Seminars.JPG
Upatikanaji wa ruzuku (Grants) kwa ajili ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na asasi za kiraia (Civil Society Organizations) imekuwa ni changamoto kubwa kwa asasi hizi. Hii hutokana na asasi nyingi kutokuwa na taarifa sahihi (accurate information) juu ya vyanzo vya ruzuku na taratibu za uombaji. Miongoni mwa makosa yafanywayo na Taasisi nyingi katika uombaji wa ruzuku ni kama ifuatavyo;

[ul]
[li]Taasisi nyingi hushindwa kutambua aina sahihi ya RUZUKU yenye kuendana na malengo ya kuanzishwa kwa taasisi zao. Kila Taasisi ina malengo yake ambayo hutimia kupitia utekelezaji wa mradi mbalimbali. Mara nyingi mfadhili anapotoa RUZUKU mfano katika eneo la UBORESHAJI SEKTA YA AFYA, basi atahitaji taasisi zenye malengo yaliyojikita kwenye masuala ya afya, ziombe fedha hizo, na si Taasisi zinazojishughulisha na masuala mengine kama vile Mazingira n.k.[/li][li]Kushindwa kuwa na mshirika sahihi (Inability to establish effective partner) Miongoni mwa vigezo vya kupata ruzuku hususani kutoka kwa wafadhili wakubwa ni Taasisi kuwa na mshirika sahihi katika utekelezaji wa mradi husika, na mara nyingi mfadhili huainisha sifa ambazo Taasisi-mshirika inapaswa kuwa nazo, kushindwa kutafuta Taasisi-mshirika yenye sifa stahiki hupelekea muombaji wa ruzuku kutokidhi vigezo na hivyo kukosa ruzuku.[/li][li]Ufahamu na uzoefu katika usimamizi wa miradi (Skills and experience on Project Management) Taasisi inaweza kuandaa andiko zuri sana la mradi (A Sound Project Proposal) kwa kumtumia mtaalamu na likapita katika baadhi ya hatua za “Evaluation” lakini isipewe fedha hizo kutokana na kutokuwa na uzoefu na ujuzi pia katika usimamiaji wa miradi. Hivyo Taasisi inapoanza shughuli zake, ni vyema ikajikita kwanza katika miradi ya kujijengea uwezo (Capacity Building Projects) ili kuwawezesha watendaji wake katika usimamiaji wa miradi.[/li][/ul]
Aina za Wafadhili wa Miradi ya Maendeleo
[ul]
[li]Official Development Assistance Agencies (ODA), kundi hili hujumuisha "agencies’ ambazo nyingi huwa chini ya wizara za mambo ya nje ya nchi zilizoendelea, mfano Australia Agency for International Development (AUSAID), Canadian International Development Agency (CIDA), the Department for International Development (DFID/UK) United States Agency for International Development (USAID) n.k[/li][li]International Nongovernmental Organizations. Haya ni mashirika makubwa na ambayo hutekeleza miradi yenye bajeti kubwa. Ili kufanikisha malengo yao, hulazimika kutoa ruzuku kwa asasi za ndani ili zitekeleze miradi katika maeneo mahsusi. Miongoni mwa mashirika haya ni Action Aid (U.K), CARE (U.S), Concern Worldwide (Ireland), Oxfam (U.K), Helvetas (Switzerland) n.k[/li][li]International Foundations, hizi taasisi zenye kujitegemea ambazo hufanya shughuli za kutoa ruzuku kwa asasi za kiraia sehemu mbalimbali duniani ili kuchochea maendeleo katika nyanja mbalimbali. Kundi hili hujumuisha Taasisi kama; Aga Khan Foundation (Switzerland), the Rockefeller Brothers Foundations (U.S), W.K Kellogg Foundation (U.S) n.k[/li][li]Aina nyingine ya wafadhili katika miradi ya maendeleo ni Balozi mbalimbali za nchi za Ulaya na Marekani, Benki za kikanda n.k[/li][/ul]

The Consult
+255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania

Kwanza tupe maoni yako kuhusu hii nugu ina jiita @T255 .