[CENTER]
Lesson Learned
So, sato niliamka bila form
Indoors, nikasema leo sidai kuroam
Kutulia tu kiasi, nikaskia phone
Nganya ya me inanicall
Kakanishow, “home kuna party”
“Pilau kwa wingi na machapati”
Heee, kusikia ati party? Machapati?
Mimi huyo, trao, viatu na shati
So, kwa matt nikaelekea kwao kejani
Kakanipick tukaingia ndani
Masalamu, nikaketi, yangu nikaletewa sahani
Kwenya ngohe, chapati, thufu na biryani
Nikajilea vizuri bila kujali
Kwa meza wakaleta wali
Bila kusleki, nikamega kaugali
Nganya ya me nikiikemba tu kwa umbali
So, nilibonya vizuri nikashiba
Tumbo furi furi bila shida
Story zikaanza, watu kujuana
Hapo ndo nikakumbuka
Heee, na si nimemanga sana
Kwanzia supu na mamutura za jana
Supper, kathembe na nyama
Breko, hivo hivo kama jana
Alafu sahi, lawama
Hapo ndo tumbo ilianza kuleta balaa
Nikajua leo nayo nimepatikana
Hapa lazima niondokee hizi jamaa
Hapa itabidii nimeunda sana
Teke, nikarauka, na kusaka mama
Nikamshow naunda, tumbo imeleta noma
Kakacheka na kunishow niache ufala
Niaje na manga alafu nadai kuhepa
Enyewe nikaona ata mimi nimeingiza za ovyo
Kakanisho, maybe nitafeel poa nikienda choo
Nakapenda, so nikagree, hio loo kakanishow
Manze hapo ndo saa maneno ilianza kuflow
Choo ilikuwa just next to sito
Nikaingia teke, nilikuwa nimekazwa vi soo
Mlango nikafunga na kuketi, ready to go
Maneno, wacha zianze kuflow
Si mchezo, nilikuwa nimemanga sana
Mizinga tu nilikuwa naangusha ka osama
Each drop, kwa moyo nikifeel, hapo sawa
Vile tu shughuli nimemada
Trao kuvaa na kupull kamba
Blunder
Tank empty, hakuna waba
Hee, sema mwanaume kutense
Stranded, already choo nimemess
Nikashindwa saa hapa what next
Kutoa simu, nganya kutext
Niaje babe, hii choo yenu haina maji
Na already nishamaliza kazi
Hakureply, nikajua hapa nayo nitatii
Vile nilikuwa narusha mizuka na bidii
What such a pity
So, kwa choo nikakaa for about an hour
Mawazo huku inanigonga sawa sawa
Aii, arufu ikazidi, nikasema hapana
Hii ni mchezo, wacha niache ufala
So, pole pole door nikafungua
Nakukemba rada kama kuna mtu najua
Hakuna raiya, wazi, mimi huyo nikajitoa
Nikeanda kusaka mama pahali alikua
Kwa harakati zangu, nganya nikaipata
But it was too late
Buda yake alikuwa asha fyetu
Alienda choo, akapata mamess tu
Hee, ka ni wewe ungefanya nini
Ju mi naye nilijifanya si mimi
Ikabidii ni watoi wamebeba musalaba
Teke teke wakaambiwa wasake waba
Hahaha, choo ilisafishwa mara moja
Despite that, sherehe ikaendelea bila hoja
Nganya yangu huku ilishinda ikinicheka
But, do I care
Lesson Learned
Ukienda party
Mizigo yako
Peleka kwako
Ama utatii
[/CENTER]