wewe ni nani?

Tuchangie kwa Umakini, eti nasikia wengine ni Wadudu na wengine wana Roho za Mashetani…!!! na Unapoulizwa Wewe ni nani wakati anakuona anamaanisha nini? kwa sababu kama ni Jina analifahamu…!!!

Tafakari kabla ya kutoa Mchango wako…

Ni kweli watu wameshindwa kujieleza kuwa wao ni nani…???Waliotazama uzi huu ni zaidi ya watu 56, aibu sana hii…!!!

http://bwaya.blogspot.com/2007/11/wewe-ni-nani.html

To know the real YOU, you have to spend more time on yourself. Take a time for a self analysis, neglect all of the external thoughts, and allow the flow of your true Identity from internal to external!!

You’re more than what you think!! By Dr Philosopher

Mimi ni binadamu

Mimi ni Smart911

Cc: @Mahondaw

Mimi ni mimi, na hakuna anayeweza kuwa mimi isipokuwa mimi mwenyewe…

Mimi slimTano

Wakuu Kylie, slim5 na Smart911 jaribuni kuneglect all of the external thoughts, and allow the flow of your true Identity from internal to external!! kwani majina, Dini nayanayofanana na hayo ni mambo ambayo uliyakuta baada ya kuzaliwa na ukalazimisha kuyafuata…!!! hebu yaache hayo yakupangiwa jibu kutokana na wewe

mkuu kidogo umejaribu ingawa kiuhalisia hujajibu umeligeuza swali kuwa jibu…!!!

Bado jibu langu litaendelea kuwa lilelile na ninao uhakika. MIMI ni mimi kwa kuwa mimi si huu mwili wala jina nililopewa au kujipa; mimi si sifa ninazopewa au kujipa; mimi si mawazo yangu; mimi si jinsi ninavyovaa, kuongea au kuandika… Mimi ni mimi (kwa maana ya andiko kutoka Mwanzo 1:26, ingawa wengi wanachanganya na Mwanzo 2:7). Ndiyo maana mwili huu ukifa hawatasema tena huyu ni Bishop bali mwili wa Bishop. Hivyo MIMI nitaendelea kuwa MIMI na hakutatokea mwingine ambaye ni mimi bali atafanana na mimi…

Hoja hii imekaa kithiolojia zaidi kuliko falsafa na inahitaji hekima za Mungu pekee kuweza kuelewa maana yake…

Unaposema Mwazo 1:26 na Mengine yanayofanana na hayo ni mapokeo ya Kithiolojia tu yaliyowekwa na usipofuata utaambiwa unamuasi Mungu…!!!

Kumbuka ukuaji wa Kiakili(Ufahamu) wa mtoto mwenye Umri hadi miaka mitatu (3) mara zote hutegemea Vitu, Mazingira yanayomzunguka, pamoja na watu. Je bila Mazingira hawezi kuwa yeye…???

Nakubaliana nawe ya kuwa Hekima inahitajika katika kulijibu swali hili na si kulielewa tu…